Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Magoli zamani hayakuwa na mwamba wa juu

Muktasari:

  • Magoli ya zamani hayakuwa na jiti au ubao wa juu na kwahivyo hata mpira uwe umeruka juu vipi katika eneo liliokuwa kati ya majiti au mabao ya pembeni basi huhesabika ni goli.

HAPO zamani magoli katika kandanda yalikuwa sababu kubwa ya kutokea mzozo na hata kupelekea mchezo kumalizika kabla ya muda uliopangwa.

Magoli ya zamani hayakuwa na jiti au ubao wa juu na kwahivyo hata mpira uwe umeruka juu vipi katika eneo liliokuwa kati ya majiti au mabao ya pembeni basi huhesabika ni goli.

Hili nalo lilizusha utata kama lile ambalo llikuwa la mwendo wa kasi na kupita pembeni huku waliokuwa wahesabike wamefungwa wakisema sio goli na wapinzani wao wakisema ni goli.

Utata huu ambao wakati mwengine ulipelekea wachezaji na mashabiki kupigana ilipelekea magoli kufanyiwa marekebisho makubwa hadi kufikia namna yanavyoonekana hii leo.

Hapo mwanzo ilikuwa haipo sheria ya upana wa goli wakati ilipokuwa inatumika miti au mbao kwa kuweka nguzo mbili na hapakuwepo mwamba uliounganisha hiyo miti au mbao.

Haikuwa jambo la ajabu katika miaka ya nyuma kukuta goli moja kuwa pana kidogo kuliko jingine au nguzo imepinda kidogo na kulifanya goli kuwa jembamba kidogo baaadhi ya sehemu.

Mwamba wa goli ulianza kuwekwa kama pendekezo katika mwaka 1875 na kuwa ni lazima kuanzia mwaka 1882 na sheria kutungwa kwa goli kuwa na upana wa futi 24 na urefu wa futi 8 kutoka chini. Kipimo hicho kinatumika hadi hii leo, lakini vipo vipimo ambavyo ni vidogo kidogo kwa magoli ya watoto, vijana na wanawake.

Katika siku za hivi karibuni baadhi ya wataalamu wa mchezo wa kandanda na wachezaji maarufu wastaafu walishauri upana wa goli uongezwe kwa futi moja na urefu kwa inchi sita, lakini pendekezo hili kila likijadiliwa matokeo yake ni kuwekwa kapuni.

Mwamba wa juu ulianza kutumika katika fainali ya Kombe la FA mwaka 1872 kati ya Wanderers na Royal Engineers kwenye Uwanja wa Kennington. Wanderers walishinda 1-0.

Lakini huu mwamba ulikuwa wa utepe wa kitambaa na ilionekana kama hatua muhimu ya kupunguza migogoro na katika mwaka 1882 utepe ukaondolewa na kuwekwa mwamba wa bao.

Hata hivyo, kuwekwa kwa mwamba wa bao hakukumaliza, bali kulipunguza matatizo.

Adhabu ya tuta (penalti) panapokuwepo mchezo mbaya ndani ya eneo la hatari haikuwepo hapo zamani. Adhabu hii ilianzishwa mwaka 1890 na William McCrum ambaye alikuwa mfanya biashara na akicheza kama golikipa.

Kuwepo kwake kulikubalika katika mkutano uliofanyika katika mkutano wa chama cha kandanda cha Shefield, England mwaka 1891 na mnamo mwaka 1902 iliingizwa rasmi katika mfumo wa kandanda na kuwekwa kipimo kinachotumika hadi sasa cha yadi 12.

Wachezaji walitakiwa wawe nje ya eneo la hatari pale penalti inapopigwa. Katika mwaka 1905, palitungwa sheria ya kumtaka golikipa asitikisike akiwa amesimama kwenye mstari wa goli mpaka mpira utapopigwa, lakini sheria hii ikafutwa na kukubaliwa katika mwaka 1997 kutikisika anavyotaka wakati penalti inataka kupigwa.

Katika mwaka 1970 pakazuka tatizo jengine katika upigaji wa penalti. Nalo ni la anayepiga mpira kusita wakati akipiga mpira, tabia iliyoanzishwa na aliyekuwa akitambulika kama Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’, ambaye aliiaga dunia mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka 82.

Kwanza ilikatazwa na ilipotokea mchezaji alitakiwa apigete na mpira, lakini baadaye umamuzi huo ukatenguliwa mnamo mwaka 1985.

Kwa miaka mingi palitumika njia mbalimbali ya kutafuta mshindi pale timu zikienda sare katika michezo ya mtoano. Hapo kwanza ilikuwa inatumika njia ya kurudiana, lakini hii nayo ilikuwa na tatizo kwa vile ilikuwa inatokea timu zinakwenda sare mara mbili hadi tatu na kutopatikana mshindi.

Kwanza pakawekwa muda wa nyongeza wa dakika 30 ziliogawiwa mapande mawili, kila moja la dakika 15 na baada kuongezewa muda wa dakika chache kwa zile ziliopotezwa kwa makusudi au kukawilisha mchezo alipotokea mchezaji kujeruhiwa au kutoelewana.

Njia moja nyingine iliyotumika ni kurusha sarafu na atakayebahatika ndio huwa mshindi. Hii ilianza kutumika mara chache sana kuanzia mwaka 1867, lakini ikapewa nguvu kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1960.

Miongoni mwa klabu ambazo zilipoteza ushindi kwa aina hii ni Yanga ya Dar es Salaam ilipotolewa na Asante Kotoko ya Ghana katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1969.

Matumizi ya sarafu kuamua mashindi yalizusha lawama nyingi na hasa katika mashindano ya Ulaya, Olimpiki na Kombe la Dunia. Baada ya mjadala mrefu ikakubaliwa mtindo wa kupiga penalti 5 baada ya kupulizwa filimbi ya kumaliza muda wa kawaida.

Katka mashindano ya Kombe la Ulaya ya 1976 ndio ukatumika mtindo huu na mchezo wa kwanza ulikuwa katika fainali kati ya Czechoslovakia na Ujerumani na Wajerumani kushinda 5-4. Katika kutafuta Kombe la Dunia ulitumika pia.

Katika historia fupi ya kutumika mtindo huu wa kupigiana matuta kupata mshindi mchezo ulioweka historia ya kuwa na penalti nyingi mpaka mshindi kupatikana ni kati ya klabu ya Dimona na Shimson Tel Aviv, zote za Israel. Palihitajika kupigwa penalti 56 ndio pakaweza kupatikana mshindi kati ya timu hizi mbili mnamo tarehe 18 Septemba, 2004.

Katika mwaka 2006, mchezo wa robo fainali za AFCON uliofanyika Misri kati ya Cameroon na Ivory Coast uliweka rekodi ya kupigiana matuta katika mashindano hayo. Ivory Coast ilishinda 12-11.

Kabla ya hapo, mnamo mwaka 1992 Ivory Coast iliifunga Ghana 11-10 katika mchezo wa fainali wa Afcon mwaka 1992 kwenye Uwanja wa Leopold Sedar Senghor uliopo Dakar, Senegal.