Ndugu wagawa familia Kombe la dunia
Muktasari:
- Kile kinachofanya hadithi hizi kuwa za kusisimua ni kwamba vijana hao wote walikua wakicheza mpira mmoja kwenye bustani na viwanja vilevile vya mazoezi. Hata hivyo, Kombe la Dunia litakapoanza, wataingia uwanjani wakiwa wamebeba bendera tofauti mabegani mwao.
LONDON, ENGLAND: MAISHA yanaweza kuwa ya ajabu, hata ya kushangaza wakati mwingine. Hilo hujitokeza hasa tunapokutana na visa vya ndugu waliozaliwa na wazazi wale wale lakini wakawakilisha nchi tofauti.
Naamini usiamini, katika Kombe hili la Dunia kutakuwa na familia tatu zilizogawanyika si kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia, bali kwa sababu ya mipaka ya kitaifa.
Kile kinachofanya hadithi hizi kuwa za kusisimua ni kwamba vijana hao wote walikua wakicheza mpira mmoja kwenye bustani na viwanja vilevile vya mazoezi. Hata hivyo, Kombe la Dunia litakapoanza, wataingia uwanjani wakiwa wamebeba bendera tofauti mabegani mwao.
Hii ni simulizi tamu ya familia hizo tatu ambazo dakika 90, tizagawanyika kutokana na vijana wao kuwa katika uwakilishi wa mataifa tofauti. Hapa chini kuna orodha ya ndugu wa damu watakaoshiriki katika mashindano hayo makubwa ya soka duniani.
Jambo la kuvutia Kombe la Dunia la 2026 linaendelea kuonyesha jinsi soka linavyounganisha familia, huku baadhi ya ndugu wakicheza pamoja katika timu moja na wengine wakikutana kama wapinzani wakiwakilisha mataifa tofauti.
1. Jurrien Timber na Quinten Timber (Uholanzi)
Ndugu hawa wote wawili wamejumuishwa katika kikosi cha Uholanzi kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Jurrien Timber anacheza nafasi ya beki, huku Quinten Timber akicheza kama kiungo wa kati.
2. Theo Hernandez na Lucas Hernandez (Ufaransa)
Ndugu wa familia ya Hernández wote ni sehemu ya kikosi cha Ufaransa katika Kombe la Dunia.
Wao ni miongoni mwa ndugu maarufu zaidi katika soka la kimataifa kutokana na mafanikio yao makubwa katika ngazi ya klabu na timu ya taifa.
3. Nico Williams na Inaki Williams
Hii ni familia yenye historia ya kipekee, kwani ndugu hawa wanawakilisha mataifa tofauti.
Nico Williams anachezea Hispania, wakati kaka yake Inaki Williams anachezea Ghana. Mataifa yote mawili yamefuzu Kombe la Dunia na wachezaji hao wamejumuishwa katika vikosi vyao.
4. Desire Doue na Guela Doue
Desire Doué ataiwakilisha Ufaransa katika Kombe la Dunia la 2026, huku kaka yake mkubwa Guela Doué akiichezea Ivory Coast.
Hivyo, kama ilivyo kwa familia ya Williams, ndugu hawa pia watakuwa wakitetea bendera za mataifa tofauti kwenye mashindano hayo makubwa.