Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SPOTI DOKTA: Siri mastaa kutumia tiba ya oksijeni

Muktasari:

  • Hawa wanamichezo hutumia tiba ya oksijeni ya ziada ili kuleta matokeo makubwa na ya haraka ikiwamo kujenga ustahimilivu, kuharakisha uponaji majeraha na kuboresha afya kwa ujumla.

TIBA ya oksijeni ya Hyperbaric kifupi HBOT hivi sasa imekuwa maarufu kwa wanamichezo duniani ikiwamo wanaocheza kandanda, kikapu, mpira wa magongo, wapiga mbizi na wanariadha.

Hawa wanamichezo hutumia tiba ya oksijeni ya ziada ili kuleta matokeo makubwa na ya haraka ikiwamo kujenga ustahimilivu, kuharakisha uponaji majeraha na kuboresha afya kwa ujumla.

Mastaa wanaomiliki kifaa hicho ambacho thamani yake ni takriban kati ya Sh300  milioni hadi milioni 500 ni pamoja na Cristiano Ronaldo, Mohamed Salah na  LeBron James wa Ligi ya Kikapu Marekani.

HBOT inatumika katika matibabu zaidi ya 200 ikiwamo kutibu majeraha mabaya, uharibifu wa tishu kutokana uvamizi wa bakteria, mtu kuvuta sumu ya carbon monoxide na majeraha ya mionzi.

Mfano mshambuliaji Gerald Mdamu aliyepata ajali 2024 na kuvunjika mguu wakati akiichezea Polisi Tanzania ni mmoja wa majeruhi ambaye angestahili kupata huduma ya HBOT ili kuwezesha jeraha lake kupona haraka.

Habari nzuri kwa Tanzania ni kuwa tayari kifaa hicho kilishazinduliwa tangu mwaka jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), na tayari wataalamu wa afya wako nje ya nchi wakisomea fani hiyo.


INAVYOFANYA KAZI

Kifaa hicho ambacho kipo kama kajichumba kenye umbile la silinda, ndani yake hutoa hewa ya oskjeni halisi ya asilimia 100 ikiwa katika shinikizo la juu mara mbili hadi tatu kuzidi shinikizo la hewa ya kawaida.

Tiba ya HBOT ilizoeleka zaidi kutumiwa na marubani, wanaanga wa safari za anga za mbali na wapiga mbizi wa kina kirefu ili kustahimili na kukabiliana na changamoto wanazopata za upungufu wa oksijeni, ikiwamo tatizo la mgandamizo na viputo vya hewa katika damu.

Kanuni ya tiba ya HBOT ni kupata oksijeni katika shinikizo la juu la hewa kwa haraka na hii ni kutokana na tabia za hewa kufyonzwa haraka na mwili  katika mazingira ya shinikizo kubwa.

Mtu huingia ndani kwa ulalo huku akivuta hewa ya oksijeni halisi na hatimaye kufika kwa wingi katika damu ambayo baadaye husambaa maeneo mbalimbali mwilini.

Kupata oksijeni kwa wingi kunawezesha kuharakisha uponaji kwa matatizo ya kiafya yenye upungufu wa hewa ya oksijeni ikiwamo majeraha makubwa ya tishu yenye uvamizi wa bakteria.

Tiba hiyo inawezesha mapafu kuchukua hewa hiyo kwa  urahisi na kwa haraka, hivyo kuingia katika damu na kufanya seli na tishu kupata oksijeni kwa wingi kuliko nje ya mashine ya Hyperbaric.

Faida kubwa ya tiba hiyo ni kusaidia damu kutiririka kwa wingi, kupunguza shambulizi la mjibizo wa kinga, kudhoofisha bakteria waliovamia, kusaidia kukabiliana na radiko huru ambazo zikirundikana huharibu seli.

Vilevile huchochea ukuaji wa mishipa mipya ya damu, kuondoa viputo vya hewa vilivyonaswa kwenye mishipa ya damu, kuzuia ugonjwa kuongezeka na kufifisha makali ya magonjwa yatokanayo na mazingira.

INATUMIKA KWA MATATIZO HAYA

1. Kusaidia majeraha kupona haraka

Inashauriwa kutibu majeraha ya michezo kwa tiba hii haraka iwezekanavyo. Uponaji utaongezeka kwa kasi ikiwa mwanamichezo atapokea matibabu ya oksijeni ya hyperbaric ndani ya saa 24 hadi 48 za kwanza. HBOT pia husaidia kupunguza uharibifu wa tishu zilizojeruhiwa.

LeBron James, mmoja wa mastaa maarufu duniani kutoka Ligi Kuu ya Kikapu (NBA) ambaye ni muumini mkubwa wa tiba ya hiyo. Nyota huyo anaitumia ili kuimarisha utendaji wa mwili na kupona vijijeraha vya ndani kwa ndani vinavyotokea wakati wa mazoezi na mechi.

Kulingana na LeBron, hutumia pia ili kusaidia mwili wake kupona haraka majeraha na kuondokana na hali ya uchovu ili hatimaye kumfanya kuwa mpya kila wakati.


2. Kuondoa maumivu na uvimbe bila dawa

Kitendo cha kuboreka na kinga ya mwili na huku pia damu yenye oksijeni nyingi kutiririka kwa wingi mwili husaidia kudhibiti mjibizo wa kinga ya mwili na hatimaye maumivu na uvimbe kuondoka.

Majeruhi anaweza kupunguza uhitaji wa dawa za maumivu kwa sababu hupona haraka majeraha. Hii ndio sababu inayochangia wanamichezo kupona kwa usalama na kwa ufanisi ili hatimaye kurudi katika mchezo wakiwa timamu.

3. Kuondoa uchovu wa mwili

Uchovu husababishwa na misuli ya mwili kufanya kazi kubwa huku kukiwa na deni la oksijeni. Mwili kupata oksijeni kwa wingi na huku ikiwa halisi, husaidia kufidia deni la oksijeni haraka hatimaye uchovu huondoka.

4. Nguvu na ustahimilivu

Kupata oksijeni kwa wingi na kwa urahisi kunafanya miili kuwa na nguvu kubwa na kufanya kazi muda mrefu bila kuchoka. Hii ni kwa sababu ya kuwa na hifadhi kubwa ya oksijeni katika mwili.


5. Kuleta usingizi mzuri

Ingawa kwa kawaida mtu halali kwenye chumba chenye hyperbaric kwa kupumzika usiku mzima, baadhi ya wanamichezo hulala kwa muda katika HBOT ili kuboresha  usingizi wa kitandani. Wingi wa oksijeni mwilini husaidia kupunguza maumivu na uchovu, kuongeza utulivu kiakili na kuboresha mifumo ya usingizi


6. Kuleta hisia nzuri

Mazingira ya kifaa hicho na kitendo cha mwili kupokea oksijeni halisi husababisha mtumiaji kuburudika na kuwa na hisia nzuri ikiwamo furaha. Pia kuondokana na uchovu humfanya mtu kuhisi kutua mzigo mwilini.


7. Kukabiliana na matatizo ya afya ya akili.

Mfano mzuri ni nyota wa muziki wa Pop, Justin Bieber amekuwa akitumia tiba ya oksijeni kwa wingi ili kuboresha afya ya akili na kukabiliana na matatizo kama vile wasiwasi na mfadhaiko.


8. Afya ya ngozi na kukabaliana uzee

Wakati wanamichezo wakitumia HBOT kukabiliana na majeraha ya michezo, mastaa wa Hollywood wanaocheza filamu, wanamitindo na mamisi huitumia kwa ajili ya kulinda afya ya ngozi na kukabiliana na hali ya uzee.