Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

STELLENBOSCH: Wasauz walioshika tiketi ya Simba fainali CAF

STELE Pict

Muktasari:

  • Simba imefuzu nusu fainali ya michuano hiyo ikiifunga Al Masry kwa penalti 4-1 baada ya matokeo ya jumla kuwa 2-2, huku Stellenbosch FC ikiwaondoa mabingwa watetezi, Zamalek kwa bao 1-0 lililofungwa na Sihle Nduli.

WANA nusu fainali wawili wanaokwenda kukutana katika Kombe la Shirikisho Afrika, Simba na Stellenbosch FC, wameweka rekodi mpya kutokana na kufika hapo kwa mara ya kwanza.

Simba imefuzu nusu fainali ya michuano hiyo ikiifunga Al Masry kwa penalti 4-1 baada ya matokeo ya jumla kuwa 2-2, huku Stellenbosch FC ikiwaondoa mabingwa watetezi, Zamalek kwa bao 1-0 lililofungwa na Sihle Nduli.

Timu hizo hii ni mara ya kwanza kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika tangu michuano hiyo kuanza rasmi mwaka 2004, hivyo kwa namna yoyote ile mojawapo itaongeza rekodi kwa kucheza fainali.

Simba inatajwa kuwa na nafasi kubwa ya kufuzu fainali kutokana na uzoefu wao wa michuano ya kimataifa tofauti na Stellenbosch ambayo hii ni mara ya kwanza kushiriki.

Mbali na timu hizo, pia RS Berkane ya Morocco itacheza dhidi ya CS Constantine kutoka Algeria katika nusu fainali nyingine.

STEL 01

STELLENBOSCH WAPOJE?

Timu hiyo inayotumia jina la mji inaotokea wa Stellenbosch, Afrika Kusini, ilianzishwa Agosti 3, 2016 na sasa inakwenda miaka tisa ya uhai wao.

Ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki michuano ya CAF, huu ni msimu wa sita kwa timu hiyo kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini.

Katika misimu mitano iliyopita, Stellenbosch nafasi ya juu zaidi kukamata kwenye Ligi Kuu ya Afrika Kusini ni ya tatu ilipofanya hivyo msimu uliopita huku 2021-2022 ikiwa ya nne, kisha 2022-2023 ikimaliza ya sita.

Msimu mbaya zaidi kwao ulikuwa wa pili ambao ni 2020-2021 ilipomaliza nafasi ya 14, wakati ule wa kwanza 2019-2020 ikikamata nafasi ya 10.

STEL 02

WACHEZAJI WA KIGENI WATANO

Katika kikosi chao kinachoundwa na nyota 30, kuna watano pekee ambao ni raia wa kigeni wakitoka nje ya Afrika Kusini ambao ni mabeki Brian Onyango (Kenya), Kazie Godswill (Nigeria), Olivier Touré (Ivory Coast) na kiungo Ibraheem Jabaar (Nigeria).

Kikosi chao hicho kina wachezaji wenye wastani wa umri wa miaka 26.1 huku nyota wanne pekee ndiyo wanacheza timu zao za taifa.

Simba ina wachezaji 12 wa kigeni huku kikosi kizima nyota 11 wamekuwa wakiitwa timu zao za taifa mara kwa mara.

STEL 03

KIKOSI CHA BILIONI 33

Katika suala la kujijenga kiuchumi, Stellenbosch ipo vizuri kwani kikosi chao kizima kina thamani ya Euro 11.4 milioni sawa na Sh33.5 bilioni za Kitanzania.

Ukija kulinganisha na Simba, thamani ya kikosi chake ni euro 2.2 milioni sawa na Sh6.4 bilioni. Hiyo ni kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarket.

STEL 04

SAFARI YAO CAF

Stellenbosch ilianzia hatua ya awali wakati Simba ikianzia hatua ya pili. Wasauz hao walianza kwa kuitoa Nsingizini Hotspurs ya Eswatini kwa jumla ya mabao 8-0, kisha ikaiondosha AS Vita Club ya DR Congo kwa jumla ya mabao 3-1.

Hatua ya makundi, ilimaliza nafasi ya pili Kundi B nyuma ya vinara RS Berkane na ilikusanya pointi tisa baada ya kushinda mechi tatu na kupoteza tatu kati ya sita ilizocheza.

Katika mechi 12 za mashindano hayo msimu huu, Stellenbosch imefunga mabao 18 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 11.

Timu hiyo inanolewa na kocha raia wa Afrika Kusini, Steve Barker mwenye umri wa miaka 57, kocha huyo amekuwa na timu tangu Julai Mosi, 2017.

STEL 05

SIMBA WANASEMAJE?

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema maandalizi ya nusu fainali hayatakuwa mteremko kwani wanakutana na Stellenbosch ambayo ni timu ngumu.

“Tunaiheshimu Stellenbosch. Ni timu nzuri, wana nidhamu, wana kasi na wana wachezaji vijana wenye njaa. Tutalazimika kuongeza kasi ya maandalizi yetu,” amesema Davids.

Abdi Banda, beki wa zamani wa Simba ambaye amewahi kucheza soka la kulipwa Afrika Kusini kwa zaidi ya miaka mitano akiwa na Baroka FC, Highlands Park, kabla ya msimu huu kutua Dodoma Jiji, ameizungumzia Stellenbosch akisema:

“Ni timu yenye nidhamu sana kiuchezaji. Wanajua kujipanga, wanacheza mpira wa haraka. Lakini Simba ni timu ya ushindani. Wachezaji wakiwa na mtazamo sahihi, wanaweza kuivunja ngome ya Stellenbosch. Suala ni kujiamini na kucheza kwa mpango.”

STEL 06

RAMANI YA FAINALI

Simba sasa inaingia kwenye orodha ya timu nne bora Afrika kwa msimu huu kwenye Kombe la Shirikisho. Mchezo ujao dhidi ya Stellenbosch utakuwa mtihani mkubwa, hasa kwa kuwa Wasauzi hao hawazungumzwi sana lakini wamewashangaza mabingwa watetetezi, Zamalek.

Nusu fainali ya kwanza Simba itakuwa mwenyeji Aprili 20, kisha marudiano Aprili 27. Endapo Simba itafuzu fainali, ile ya kwanza itaanzia ugenini Mei 17 na marudiano Mei 25 nyumbani.

“Tunataka zaidi. Tumefika hapa kwa damu, jasho na machozi. Hatutarudi nyuma,” amehitimisha Fadlu.