Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

#WC2018: Mademu bomba wanaowapa moto mastaa wa England

Muktasari:

  • Kama hilo lisemwalo ni kweli, basi litakuwa linawahusu moja kwa moja mastaa wa timu ya taifa ya England.

ETI wanasema hivi, kila kwenye mwanamume mwenye mafanikio, nyuma yake kuna mwanamke shupavu.

Kama hilo lisemwalo ni kweli, basi litakuwa linawahusu moja kwa moja mastaa wa timu ya taifa ya England.

England kwa mara ya kwanza wamekwepa jinamizi la kuchapwa kwenye mikwaju ya penalti katika fainali za Kombe la Dunia, baada ya juzi Jumanne kuwachapa Colombia kwa penalti 4-3 katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya fainali hizo za Kombe la Dunia 2018 huko Russia na kutinga hatua ya robo fainali.

Kwenye fainali za Kombe la Dunia 2010, aliyekuwa kocha wa England wakati huo, Fabio Capello aliwapiga marufuku wanawake wa wachezaji kwenda Afrika Kusini na timu hiyo, lakini kocha wa sasa Gareth Southgate ametoa ruhusa wachezaji wake wakutane tu na wake na wachumba zao hotelini kila baada ya mechi ili kujiliwaza na ndiyo maana kuna utulivu mkubwa sana wa kikosi cha Three Lions katika fainali hizo za Russia.

Hii hapa orodha ya wanawake matata wanaotia chaji mastaa wa England na kuwafanya kuwa na imani kubwa ni wakati wao wa kubeba ubingwa wa fainali hizo za Kombe la Dunia linaloendelea huko Russia, ambako kwa sasa limefikia kwenye hatua ya robo fainali. Hii ni wale walioanzishwa kwenye mechi dhidi ya Colombia.

Megan Davison (Jordan

Pickford)

Kipa, Jordan Pickford alicheza penalti moja kuwafanya England kuibuka na ushindi, hivyo kutinga hatua ya robo fainali huko Russia. Nguvu ya Pickford ilikuwa ikichagizwa na mrembo matata, Megan Davison, ambaye ndiye kipenzi cha roho yake tangu wakiwa watoto.

Wawili hao walikutana kipindi hicho wakiwa na umri wa miaka 14. Megan ni mhitimu wa elimu ya chuo kikuu.

Annie Kilner

(Kyle Walker)

Mtindo wa England kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 ni kutumia mabeki wa kati watatu na hapo ndipo anapotumika Kyle Walker, ambaye kimsingi ni beki wa pembeni.

Kiwango cha Walker kimekuwa matata kabisa kwenye fainali hizo, lakini inaelezwa nguvu na sababu ya kupambana anaipata kwa mrembo wake matata kabisa, Annie Kilner. Wawili hao wamefanikiwa kuwa na mtoto mmoja wa kiume, Riaan.

Mille Savage

(John Stones)

Beki mwingine wa kati kwenye kikosi cha England, aliyeanzishwa kwenye mechi hiyo dhidi ya Colombia ni John Stones. Staa huyo wa Manchester City amekuwa akitamba kweli kweli kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Russia na pengine hilo linatokana na kuwa na uhakika anashangiliwa na kipenzi chake, mrembo Millie Savage.

Wawili hao wamekuwa pamoja tangu walipokuwa na umri wa miaka 12 na hata kuchorana tattoo kuonyesha mahaba yao.

Fern Hawkins

(Harry Maguire)

Beki wa kati, Harry Maguire ni moja ya nguzo imara kabisa kwenye safu ya ulinzi katika kikosi cha England huko Russia. Kwa sasa wametinga hatua ya robo fainali na hilo kwa namna moja au nyingine limechangia kuifikisha timu hiyo ilipofika kwa sasa.

Lakini, unaambiwa hivi Maguire mwenyewe ujanja wake wote upo kwa mrembo Fern Hawkins, hapindui huko na ndiko kunakompa mzuka wa kufanya vizuri zaidi ndani ya uwanja. Wapo pamoja kwa miaka saba sasa.

Nicky Pike

(Ashley Young)

Miaka minne iliyopita kama kuna mtu angesema Ashley Young siku moja atakuja kuwa beki wa kushoto chaguo la kwanza kwenye kikosi cha England, wengi wangekucheka tu.

Lakini, kwa wakati huu unaposoma hapa, Young ndiye chaguo la kwanza la beki wa kushoto kwenye kikosi cha England kilichopo huko Russia kwenye Kombe la Dunia.

Hata hivyo, unaambiwa kutamba kwa mchezaji huyo kunatokana na tulizo la moyo analopata kutoka kwa mrembo Nicky Pike.

Charlotte Trippier (Kieran Trippier)

Mrembo Charlotte Trippier yupo Russia kwenye fainali za Kombe la Dunia kumpa mzuka kipenzi chake cha moyo, Kieran Trippier. Jambo hilo limemfanya beki huyo wa kulia kucheza kwa kiwango kikubwa sana na alikuwa wa kwanza kumfariji mpenzi wake baada ya kukumbana na kipigo kutoka kwa Ubelgiji.

Charlotte anampa utulivu Trippier ambao unamfanya akili yake aielekeze ndani ya uwanja tu kuisaidia timu yake ya taifa ya England.

Rebecca Burnett

(Jordan Henderson)

Ujanja wote wa kiungo, Jordan Henderson unasababishwa na mrembo matata, Rebecca Burnett, Mrembo Rebecca amemfanya Henderson kuwa mtu wa kujali familia yake zaidi na ndiyo maana muda mwingi wamekuwa pamoja na kufurahia maisha yao.

Wawili hao wamefanikiwa kupata watoto wawili, ambao ni Elaxa na Alba, lakini kubwa ni utulivu anaopata Henderson kutoka kwa mkewe kumfanya atulize akili yake ndani ya uwanja kuipa England ushindi.

Ruby Mae

(Dele Alli)

Kiungo Dele Alli asali wake wa moyo ni Ruby Mae na mrembo huyo amekuwa akiandamana na kipenzi chake kwenye michuano yote mikubwa inayohusu timu ya taifa na waliwahi kuwa pamoja kwenye Euro 2016 na sasa wapo wote kwenye Kombe la Dunia 2018.

Ruby, ndio kitu kinachompa Dele Alli nguvu na sababu ya kupambana kwa sababu imekuwa jambo la kawaida kuwaona wakimwagiana mabusu kila baada ya mechi inapomalizika.

Jena Frumes

(Jesse Lingard)

Kuna wakati Jesse Lingard penzi lake na mrembo Jena Frumes lilitingishika baada ya staa huyo kudaiwa kuchepuka. Lakini, yote kwa yote mambo yaliwekwa vizuri na staa huyo wa England, ambaye alianza kwenye mechi dhidi ya Colombia na kuisaidia England kushinda na kutinga hatua ya robo fainali.

Mambo yao yapo vizuri na anampa sababu mchezaji huyo kutamba zaidi kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia huko Russia.

Paige Milian (Raheem Sterling)

Staa mwingine wa England, aliyeanzishwa kwenye mechi hiyo dhidi ya Colombia ni Raheem Sterling.

Kiwango chake kimekuwa kwenye ubora mkubwa kabisa kwa miaka ya karibuni na kuendeleza moto kwenye fainali za Kombe la Dunia huko Russia.

Hata hivyo, unaambiwa, Sterling anafanya vizuri kwa sababu ya kutokuwa na stresi kutokana na mapenzi ya dhati anayopata kutoka kwa mrembo Paige Milian.

Wawili hao wana mtoto mmoja wa kiume, aitwaye Thiago.

Katie Goodland (Harry Kane)

Straika Harry Kane ndiye kinara wa mabao kwenye fainali za Kombe la Dunia huko Russia baada ya kutupia wavuni mara sita hadi sasa.

Hata hivyo, makali ya mshambuliaji huyo yanatokana na utulivu wa moyo anaopata kutoka kwa kipenzi chake, mrembo Katie Goodland. Wawili hao, wamekuwa pamoja kwenye mahaba tangu wakiwa shule. Pengine Kane kwa sasa anafanya vizuri uwanjani huku mchumba wake huyo akiripotiwa kuwa mjamzito. Wana mtoto aitwaye Ivy.

Waliokuwa kwenye benchi

Kwa mastaa wa England waliokuwa benchi na kucheza kwenye mechi hiyo ya juzi, wapo kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia 2018 huko Russia wakipewa nguvu na wake na wachumba zao ambapo ni pamoja na mrembo Rebekah Vardy wa Jamie Vardy, Annabel Peyton wa Jack Butland, Gemma Acton wa Gary Cahill, Daniela Casal wa kiungo Eric Dier, aliyefunga penalti ya ushindi, Kaya Hall wa Phil Jones na wengineo kibao ambao kazi yao ni kuwafanya waume zao kutuliza akili na kuhakikisha England inabeba ubingwa wake wa dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1966. Kwenye hatua ya robo fainali, England itakipiga na Sweden.