Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Simba, amtibulia Sven

MIPANGO ya Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck kuelekea pambano lao la kiporo dhidi ya Ruvu Shooting imetibuka baada ya kuumia kwa kiungo Jonas Mkude ambaye bado haijafahamika atakuwa nje kwa muda gani kutokana na jeraha alililopata.

Licha ya kuwa na watu kadhaa wa kuziba nafasi ya Mkude akiwamo Brazili Gerson Fraga na Mzamiru Yassin, kocha Sven amekiri kuumia kwa kiungo huyo mkabaji na mchezaji mwandamizi ya Simba ni pigo kwake.

Sven alisema jopo la madaktari wa timu pamoja na waliokuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wanapambana kuhakikisha Mkude anarudi mapema kikosini, japo mpaka jana wakati anazungumza na wanahabari baada ya mazoezi ya timu yake hakuwa na majibu kamili ya tatizo la Mkude.

Kocha huyo Mbelgiji alisema Mkude amefanyiwa vipimo vya awali, lakini majibu yake bado hayajapatikana na kudai atafanyiwa vipimo zaidi kubaini tatizo lililomkubwa kwenye mguu wake wa kulia.

“Baada ya hapo ndio tutafahamu atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani na aina gani ya tiba atakayopewa, ndio maana hata katika mazoezi ya leo (jana) Jumatano hakuwepo,” alisema Sven na kuongeza;

“Kiukweli kwa namna alivyokuwa akiugulia, huwezi kumfanyia vipimo na matibabu ya haraka haraka ili aweze kucheza tutapambana ili kubaini tatizo na kumpatia tiba aweze kurudi uwanjani haraka akiwa fiti.”

“Sioni nafasi yake ya kucheza mechi dhidi ya Ruvu Shooting.”

MSIKIE MKUDE

“Sipo poa kabisa ila nashukuru Mungu nimeanza tiba ya awali huku nikifanya vipimo zaidi kubaini tatizo na matibabu mengine,” alisema Mkude mwenye mabao mawili katika Ligi Kuu msimu huu.