Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajibu apewa masharti manne

Muktasari:

  • BEKI mahiri wa aliyewahi kuwika na Yanga, John Mwansasu amemshauri winga wa Simba, Ibrahim Ajibu na kumpa masharti manne ambayo akiyazingatia yatamvusha.

BEKI mahiri wa aliyewahi kuwika na Yanga, John Mwansasu amemshauri winga wa Simba, Ibrahim Ajibu na kumpa masharti manne ambayo akiyazingatia yatamvusha.

Mwansasu alisema bado ana imani kubwa na Ajibu, endapo kama ataanza kuishi maisha yanayoustahili mpira ambayo ni kujibidiisha katika mazoezi, fitinesi, umakini na nidhamu.

Alisema akianza na hivyo atarejea kwenye ubora wake utakayomfanya agombaniwe na klabu za ndani na nje ya nchi zitakazokuwa zinahitaji faida za kipaji chake, la sivyo anaona anaweza akaondoka kwenye mstari kabisa wa wachezaji wanaotakiwa kupewa thamani kubwa.

“Wachezaji wa siku hizi na sio Ajibu peke yake sijui ni mabishoo, unakuta anakwenda mazoezini lakini anafutafuta viatu, ukiwachunguza vizuri tangu wanashuka kwenye gari hadi wanaingia uwanjani utagundua vitu vingi ambavyo unaona wanajisahau na kulewa sifa zinazowaondoa kwenye mstari

“Ajibu amezaliwa na kipaji cha mpira, angefanya bidii kwasasa angekuwa anazungumza kama mchezaji ghali, lakini anasugua benchi inakuwa ngumu hata kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars, kocha anawaita wanaoanza kikosi cha kwanza na wanaonyesha uwezo kama Mzamiru Yassin, John Bocco na wengineo, hilo linapaswa kuwa funzo kwao,” alisema.

Mwansasu alitoa ushauri wa jumla kwa wachezaji wenye vipaji waliopo Simba na Yanga, wanatakiwa kufanya mazoezi zaidi ya wale ambao wanaanza kwenye vikosi vya kwanza, ili makocha wao wanapowapa nafasi waone kitu kipya kwao.

“Nakumbuka kipindi tunacheza na kina Emmanuel Gabriel na wengine ambao walikuwa na vipaji vya juu, tulikuwa tukiingia uwanjani mashabiki wanakuwa wanajua kazi ipo na wanafurahia shoo, lakini sasa wanapata pesa ila ukiangalia leo wanacheza hivi kesho vile wabadilike,” alisema.