Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AKILI ZA KIJIWENI: Salamu za kijiwe kwa Singida Black Stars

SINGIDA Pict

Muktasari:

  • Ndani ya waraka huu kuna pongezi kutokana na mambo mazuri baadhi ambayo Singida Black Stars imeyafanya lakini upo pia ushauri wa kijiwe kwenda kwa timu hiyo inayoipa heshima kanda ya kati hivi sasa na kurejea zama zile za kina CDA aka Watoto wa Nyumbani.

WARAKA huu unatoka hapa kijiweni kwenda kwa chui wa Singida, timu ya Singida Black Stars inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa pili sasa.

Ndani ya waraka huu kuna pongezi kutokana na mambo mazuri baadhi ambayo Singida Black Stars imeyafanya lakini upo pia ushauri wa kijiwe kwenda kwa timu hiyo inayoipa heshima kanda ya kati hivi sasa na kurejea zama zile za kina CDA aka Watoto wa Nyumbani.

Kijiwe kinaipongeza Singida Black Stars kwa kutengeneza na kuzindua uwanja wake ambapo unazidi kupunguza changamoto ya viwanja bora vya soka ambayo inalikabili soka letu kwa muda mrefu hasa huko mikoani hivyo ni jambo kubwa imelifanya.

Lakini pia pongezi nyingine za kijiwe kwenda kwa Singida Black Stars ni namna ambavyo imekuwa na mwenendo mzuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo hadi sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo na kuna uwezekano mkubwa ikamaliza katika Top Four.

Kufanya huko vizuri kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na ubora wa kikosi chake ambacho kina wachezaji mafundi hasa wa mpira ambao wengi wanaweza kupata namba hata katika vikosi vya timu kubwa na pendwa nchini hivyo hapa napo kijiwe kinaipongeza Singida Black Stars.

Ushauri wa kijiwe kwa Singida Black Stars ni kwamba inatakiwa ihakikishe inafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ambayo ina uwezekano mkubwa wa kushiriki msimu ujao ama kwa kupitia tiketi ya ubingwa ya Kombe la Shirikisho la TFF au kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.

Haipaswi kuwa na ugeni kwenye mashindano hayo kama ikipata nafasi hiyo kwa vile wana timu nzuri inayoweza kumudu ushindani wa timu kutoka nchi nyingi Afrika lakini pia wana msuli wa kiuchumi wa kuwawezesha kumudu gharama za ushiriki wa mashindano ya klabu Afrika.

Utetezi wa ugeni kwenye mashindano haupaswi kuwekwa mbele hapo baadaye kwa vile soka la Afrika limebadilika siku hizi na timu nyingi mpya na zisizo na uzoefu zinafanya vizuri ilimradi tu zikiwa na vikosi vizuri.

Kama Namungo FC iliweza kipindi cha nyuma ikiwa na wachezaji wa daraja la kawaida, sidhani kama Singida Black Stars itashindwa ikiwa na hao kina Damaro, Kayekeh, Rupia na Jonathan Sowah.