Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam FC ubingwa inautaka Bara

Azam Pict

Muktasari:

  • Azam ipo nafasi ya tatu katika msimamo baada ya kukusanya pointi 36 ikiwa mbele mchezo mmoja dhidi ya Simba (40) na Yanga (39) ambazo pia zimemuacha.

KOCHA wa Azam, Rachid Taoussi amesema licha ya kudondosha pointi nyingi duru la kwanza ana nafasi ya kuipambania timu hiyo kutwaa taji msimu huu, huku akidai wazi kuwa ana pointi sita kwa  Simba na Yanga.

Azam ipo nafasi ya tatu katika msimamo baada ya kukusanya pointi 36 ikiwa mbele mchezo mmoja dhidi ya Simba (40) na Yanga (39) ambazo pia zimemuacha.

Akizungumza na Mwanaspoti, Taoussi alisema duru la pili lalasalama kila timu inahitaji kukusanya pointi tatu kila mchezo ili kujiweka kwenye mazingira mazuri mwisho wa msimu na Azam wanapambana kuhakikisha wanatimiza lengo  la kutwaa ubingwa.

“Kudondosha pointi mzunguko wa kwanza haina maana tumeshakata tamaa. Bado tuna nafasi na ukizingatia washindani wetu tuna mechi nao mzunguko huu wa pili hatuwezi kufanya makosa kudondosha tena dhidi yao hasa kwa Simba ambayo ilitufunga mzunguko wa kwanza,” alisema.

“Ukitaka kushinda taji usikubali kuwa mnyonge mbele ya mshindani wako, pointi nne ambazo wapo mbele yetu vinara wa ligi tatu tutazichukua kwao na upande wa mabingwa watetezi pia ambao wanapambania kutetea taji lao tutahakikisha tunaendelea tulipoishia.”

Azam mchezo wa kwanza inaanza dhidi ya KMC kitu ambacho kimemuibua Taoussi ambaye amesema ni ratiba nzuri kwake kuanzia nyumbani ili kutumia vyema uwanja wake kabla ya kumkabili mpinzani ugenini.