Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bajaji SpotPesa yatua Kigoma

Muktasari:

  • Mkazi wa Kigoma Hamis Kanuma amefanikiwa kushinda mchongo wa kijanja wa promosheni ya shinda zaidi ya Sportpesa.
  • Mshindi huyo alisema ataitumia kuendesha maisha yake kutokana na kipato atakachokuwa anavuna kupitia Bajaji hiyo.

MCHONGO wa kijanja wa promosheni ya Shinda Zaidi ya SportPesa umehamia mikoani, baada ya Mkazi wa Kigoma, Hamis Kanuma kunyakua Bajaj katika droo ya nne ya promosheni hiyo inayozidi kushika kwa kasi nchini.

Yanki huyo mwenye umri wa miaka 19, alisema ataitumia Bajaji hiyo ili kupiga pesa kijanja kwani hakutarajia kama ataangukiwa na zali hilo.

“Nimefurahi kushinda Bajaji ya SportPesa, hata mama yangu amefurahi sana, ninaamini itatusaidia kuinua maisha yetu,” alisema Kanuma.

“Nitaiendesha mwenyewe, natarajia kuitumia kufanya biashara na kuinua maisha yangu,” aliongeza mshindi huyo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Bajaji ya SportPesa kupata mshindi kutoka Kigoma, kwani katika droo tatu za awali mbili zilibaki Dar na moja ilienda Pangani, Tanga.

Kwa sasa mteja wa SportPesa anamaliza kazi zote kupitia menu ya kampuni hiyo kwa kutumia buku tu, kujisajili kisha kubashi michezo mbalimbali na kusubiria tu kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwamo Bajaji 100 zinazoshindaniwa.