Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Banda aiponza Richard Bay, kisa Sh 360 Milioni

BANDA Pict
BANDA Pict

Muktasari:

  • Banda kwa sasa anaitumikia Dodoma Jiji ya Tanzania kwa mkataba wa miezi sita baada ya kuvunja mkataba wake na Baroka FC ya Afrika Kusini.

RICHARD Bay ya Afrika Kusini aliyowahi kuichezea Beki Kisiki Mtanzania, Abdi Banda imefungiwa moja kwa moja kusajili wachezaji wa ndani na nje hadi itakapomlipa nyota huyo Milioni 360 za mishahara na usajili.

Banda kwa sasa anaitumikia Dodoma Jiji ya Tanzania kwa mkataba wa miezi sita baada ya kuvunja mkataba wake na Baroka FC ya Afrika Kusini.

Akizungumza na Mwanaspoti, Msimamizi wa mchezaji huyo, Fadhili Omary Sizya alisema Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) ilitoa siku 45 za kuhakikisha timu hiyo inamlipa kitasa hicho pesa zake.

"Alishinda kesi mara ya kwanza na FIFA ilitoa siku 45 zikapita bila kumlipa kwa hivyo wamefungiwa moja kwa moja, taarifa mpya ni kwamba hawatasajili hadi wamalizane na Banda pesa zake," alisema Sizya na kuongeza

"Anadai Milioni 360 bado hajaingiziwa na FIFA juzi wametoa barua ya kukumbusha kwamba siku zimepita na sasa hawatasajili mchezaji yeyote wa ndani na nje."

Mchezaji huyo wa zamani wa Simba aliichezea timu hiyo msimu uliopita kabla ya kurejea Baroka FC ambako hakupata nafasi kubwa ya kucheza kwani ndani ya msimu huo alicheza mechi nane za mashindano yote.

Banda aliwasilisha malalamiko kwa chombo cha kusimamia malalamiko ya mikataba kwa wachezaji (Dispute Resolution Chamber, DRC) Novemba 21 mwaka huu dhidi ya klabu hiyo kwa madai ya kuvunjiwa mkataba wake.

Hatua ya Banda ya kufikisha suala hilo FIFA ilikuja baada ya changamoto alizokutana nazo akiwa klabuni ikiwemo kutolipwa mishahara na ukosefu wa nafasi za kutosha za kucheza.

Hii sio mara ya kwanza kwa Banda kukumbana na kesi hiyo kwani msimu 2023 akiwa na Chippa United ya nchini humo alifungua kesi ya madai baada ya timu hiyo kuvunja mkataba wake mapema mwaka mmoja tu baada ya kujiunga.

Chippa ilishindwa kumlipa Mtanzania huyo kwa muda uliopangwa kiasi cha Sh 180 milioni jambo lililoifanya klabu hiyo kupigwa rungu la kusajili wachezaji baadae walitatua na Januari ikafunguliwa adhabu hiyo.