Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Camara atibuliwa Simba

Muktasari:

  • Camara aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Horoya AC ya kwao Guinea, amemaliza ligi akiwa kinara wa makipa ambao hawajaruhusu mabao mengi zaidi akifanya hivyo mara 19, akishindwa kuivuka rekodi iliyowekwa na Aishi Manula msimu wa 2017-2018.

KITENDO cha kipa wa Simba, Moussa Camara kuruhusu mabao mawili katika mechi ya Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga, kimemfanya nyota huyo kushindwa kuandika rekodi mpya ya kumaliza msimu akiwa na ‘clean sheets’ nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu Bara.

Camara aliyejiunga na Simba msimu huu akitokea Horoya AC ya kwao Guinea, amemaliza ligi akiwa kinara wa makipa ambao hawajaruhusu mabao mengi zaidi akifanya hivyo mara 19, akishindwa kuivuka rekodi iliyowekwa na Aishi Manula msimu wa 2017-2018.

Msimu huo wa 2017-2018, Manula aliyejiunga na Simba Agosti 9, 2017 akitokea Azam FC, alimaliza na clean sheets pia 19 kama ilivyokuwa kwa Camara ambaye ameshindwa kuandika rekodi mpya kikosini humo.

Katika mechi ya juzi iliyomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-0, nyota aliyemtibulia rekodi hiyo ni kiungo, Pacome Zouzoua aliyefunga kwa penalti dakika ya 66, baada ya kufanyiwa madhambi akiwa eneo la hatari na kipa huyo wa Simba, Camara.

Kama haitoshi, Pacome akaendelea kumtia machungu Camara baada ya kuasisti bao la pili lililofungwa na Clement Mzize dakika ya 86, likiwa ni la 14 kwake msimu huu kwenye ligi na la kwanza kwenye mechi ya Dabi ya Kariakoo.

Manula anayetajwa kwa sasa kurejea Azam, msimu wa 2017-2018 mbali na tuzo ya kipa bora aliyoshinda, aliiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, baada ya kumaliza kinara kufuatia kukusanya pointi 69.

Msimu wa 2017-2018, Manula alicheza mechi zote 30 za Ligi Kuu za Simba, japo kwa upande wa Camara msimu huu amecheza 28 na kukosekana mbili tu, sawa na kukichezea kikosi hicho cha Msimbazi kwa dakika 2520, ikiwa ndio msimu wake wa kwanza.