Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM kutafakari kuhusu viwanja vyake

CCM Pict

Muktasari:

  • CCM inakuja na kauli hiyo, wakati ambao kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau, wakihoji inawezekanaje Serikali igharimie matengenezo ya viwanja vinavyomilikiwa na chama hicho.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinafikiria kuona iwapo kiendelee kuviendesha viwanja vyake vya soka au kitafutwe mwekezaji wa kuifanya kazi hiyo.

CCM inakuja na kauli hiyo, wakati ambao kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau, wakihoji inawezekanaje Serikali igharimie matengenezo ya viwanja vinavyomilikiwa na chama hicho.

Hayo yameelezwa leo, Ijumaa Februari 21, 2025 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla alipofanyiwa mahojiano na gazeti hili.

Sababu ya kufikiri hilo, ni kile alichofafanua, gharama za kuhudumia kiwanja katika mechi moja, inazidi kiwango cha fedha inayolipwa kwa mchezo mmoja.

“Unatumia maji kumwagilia unaambiwa mechi itachezwa CCM Kirumba, bili ya maji ya kumwagilia uwanja na utaratibu uliowekwa na TFF unakuja kupewa fedha hazitoshi hata gharama za utunzaji wa uwanja,” amesema.

Kutokana na hilo, amesema ndio maana CCM inafikiri kuona iwapo inapaswa kuendelea kuviendesha viwanja au itafute wawekezaji wa kushirikiana na chama hicho kuviendesha.

“Ni mjadala lakini lengo ni kuhakikisha viwanja hivi vinaendelea kuwa katika viwango vizuri, lakini nikiri gharama za matunzo ya hivi viwanja ni kubwa mno kuliko mapato yanayopatikana,” amesema.

Hata hivyo, amesema bado hakujafanywa uamuzi kuhusu hilo, ndani ya CCM ingawa linaendelea kutazamwa kwa ajili ya hatua za baadaye.

Hata hivyo, amesema kwa sasa chama hicho kimekuwa kikishirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhakikisha viwanja hivyo vinaendelea kutumika katika mchezo wa soka.

“Kwa maana viwanja hasa vya Serikali havipo. Kwa hiyo kwa ligi yetu ilivyokuwa, CCM ikajitenga na TFF michezo ingefanyikia wapi?” amehoji.