Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chipukizi, New Kings bado zina nafasi ZPL

CHIPUKIZI Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa timu tatu tayari zimeshuka daraja ambazo ni Junguni, New Stone Town na Malindi, huku nafasi moja pekee ikisalia kukamilisha idadi ya timu nne zitakazoshuka mwishoni mwa msimu.

USHINDI wa bao 1-0 wa Polisi dhidi ya Chipukizi katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar uliochezwa Uwanja wa Gombani, Pemba, umeongeza presha kwa Chipukizi na New Kings katika vita vya kujiokoa kushuka daraja.

Matokeo hayo yameifanya Polisi kujinasua kutoka eneo la hatari na kupanda hadi nafasi ya 12 kutoka ya 13, huku New Kings ikishuka hadi nafasi ya 13.

Chipukizi bado ina nafasi ya kujinusuru endapo itashinda mechi mbili kati ya tatu zilizosalia kisiwani Pemba, jambo litakalozidisha presha kwa New Kings.

Aidha, Polisi ikifanikiwa kuifunga Junguni itafikisha pointi 38. Kisha ikishinda mechi nyingine moja dhidi ya Mafunzo au Kipanga, itakusanya alama 41 ambazo zinaweza kuifanya kubaki Ligi Kuu.

Juni 3, 2026, Chipukizi itavaana na mabingwa watetezi Mlandege, huku New King ikicheza dhidi ya Uhamiaji ambao nao unahitaji ushindi baada ya kukosa matokeo mazuri katika mechi sita mfululizo. Ushindi wa Polisi pia umeihakikishia Malindi kushuka rasmi daraja na msimu ujao kucheza Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja.

Hadi sasa timu tatu tayari zimeshuka daraja ambazo ni Junguni, New Stone Town na Malindi, huku nafasi moja pekee ikisalia kukamilisha idadi ya timu nne zitakazoshuka mwishoni mwa msimu.