Cholemelo aomba sapoti ya wadau 'Tembo Warriors'

WAKATI Timu ya taifa ya walemavu 'Tembo Warriors' ikiwa inajiandaa kurejea kambini mwishoni mwa mwezi huu, mchezaji wa timu hiyo Ramadhani Cholemelo 'Chama' amewataka wadau wa michezo nchini kuwageukia na kuwapa sapoti ya hali na mali.
Nyota huyo wa klabu ya Lester senior league L.S.L ambao ndio mabingwa mara mbili mfululizo wa Ligi ya walemavu nchini ameliambia mwanaspoti kuwa kama wadau wataishika mkono timu ya taifa basi wanaaminin watafika mbali.
"Sina hofu na kikosi chetu pamoja na benchi la ufundi lakini bado nina wasiwasi na changamoto mbalimbli ambazo hua tunakabiliana nazo ndani na nje ya uwanja na ndizo hua zinatukwamisha kufika mbali zaidi"
"Ingawa Uongozi wa shirikisho letu la soka la walamavu limekua likijitahidi sana kupambana nazo na ninawapongeza kwahilo kwani kupitia wao kuna mahali tunaona tunaweza kufiki katika soka la walemavu,"aliendelea na kusema kuwa;
"Hivyo basi nawaomba wadau mbalimbali waanze kuugeukia mchezo wetu na kutupa sapoti yao kwani kama wakitushika mkono tutaweza kufika mbali hasa katika kipindi hiki ambacho tunajianda na kushiriki kombe la Dunia"alisema Ramadhani Chomelo
Ramadhani Chomelo 'chama' alianza kuitumikia warriors mwaka 2019 na kushiriki katika michuano mbalimbali yakiwemo yale ya michuano ya Mataifa ya Afrika ya soka la walemavu (Canaf)2021 na 2019.