Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Clara Luvanga avunja rekodi yake Saudia

Clara Pict

Muktasari:

  • Kwa sasa ndiye mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo ambayo kwa upande wa wanaume yupo staa wa Ureno Cristiano Ronaldo.

MSHAMBULIAJI wa Al Nassr inayoshiriki Ligi ya Wanawake nchini Saudia, Clara Luvanga amevunja rekodi ya msimu uliopita wa kufunga mabao 12.

Kwa sasa ndiye mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo ambayo kwa upande wa wanaume yupo staa wa Ureno Cristiano Ronaldo.

Hadi sasa mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga amefunga hat-trick mbili -- moja dhidi ya Al Ula na Eastern Flames, chama la zamani la Mtanzania mwenzake Enekia Lunyamila.

Msimu uliopita Luvanga alimaliza msimu na mabao 11 akimaliza kinara wa mabao kwa upande wa Al Nassr.

Huenda msimu huu ukawa bora zaidi kwa Luvanga ambaye anatazamwa kama Ronaldo wa kike kwenye klabu hiyo.

Zikiwa zimechezwa mechi 13 za Ligi hiyo na mabingwa hao watetezi wako kileleni na pointi 39.