Coastal Union yaishusha KenGold, yatangulia Championship

Muktasari:
- Timu hiyo ilipanda Ligi Kuu msimu huu na sasa imekuwa ya kwanza kushuka daraja ikiwa na mechi tatu mkononi ambazo hata ikishinda itafikisha pointi 25 ambazo zitaibakisha nafasi mbili za mkiani.
Ken Gold imeshuka rasmi Ligi Kuu Bara baada ya kupoteza mchezo wake wa leo dhidi ya Coastal Union kwa mabao 2-1 uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Matokeo hayo yanaifanya kubaki mkiani kwa pointi 16 ikiwa na michezo mitatu ambayo hata ikishinda yote haitatoka katika nafasi mbili za mkiani.
Katika mechi tatu zilizobaki, Ken Gold itacheza nyumbani dhidi ya Pamba Jiji na Simba kisha kumalizia msimu ugenini kukipiga dhidi ya Namungo.
Timu hiyo ya mkoani Mbeya iliweka rekodi ya kumaliza kinara na bingwa wa Championship msimu uliopita na sasa inarejea tena huko msimu ujao.