Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hassan Waziri afichua kilichomplekea ulingoni

Muktasari:

  • Bondia huyo anasema tukio hilo lilimshawishi kujitosa kwenye ngumi.

Tanga ni miongoni mwa mikoa ambayo imefanikiwa kuzalisha vipaji vya mchezo wa ngumi.

Mkoa huo ndio anapotokea bondia chipukizi wa ngumi za kulipwa, Hassan Waziri ambaye yupo chini ya menejimenti ya Mitra Sport Promotion iliyoandaa pambano la Ngumi Kitaa litakalopigwa Aprili 26, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem.

Waziri ana rekodi ya kucheza jumla ya mapambano nane ambayo amefanikiwa kushinda sita kati ya hayo matatu ni kwa Knockout na amepigwa mara moja wakati pia akitoka sare moja.

Bondia huyo anayecheza katika uzani wa light anakamata nafasi ya tisa katika mabondia 118 wa uzani wake wakati duniania akiwa bondia wa 486 katika mabondia 2503.

Spoti Mikiki limefanya mahojiano na bondia huyo ambaye ameeleza kuwa ugumu wa maisha ndio ulichangia kwa kikubwa aingie kwenye masumbwi.

“Sababu kubwa ambayo imepelekea kuwa bondia ni ugumu wa maisha na kazi za kufanya hazikuwepo kabisa na niliona ngumi ni fursa za kumpatia mtu ajira.

“Lakini nakumbuka wakati nasoma tulikuwa na kawaida ya kukaa chimbo maeneo ya fukwe za bahari, Tanga nikawa namuona Allan Kamote akifanya mazoezi. Ile hali ya yeye kufanya mazoezi na nilikuwa najua yeye ni bondia ikawa inanivutia lakini kuna siku tulienda kwenye muziki na rafiki yangu ukatokea ugomvi wa rafiki yangu kugombea msichana.

“Sasa katika ugomvi nikaingilia kumsaidia rafiki yangu, nikapigwa vibaya sana lakini katika tukio lile Allan Kamote alikuwepo na yeye akaingilia kuamulia ugomvi na kutuambia ngumi za mtaani siyo nzuri kabisa, tuache,” anasema Waziri.

Bondia huyo anasema tukio hilo lilimshawishi kujitosa kwenye ngumi.

“Nilimfuata (Kamote) kumueleza kuwa nataka nijifunze kupigana ila alinimbia nishirikishe wazazi wangu. Wazazi wakanikatalia kwa sababu nilikuwa bado mdogo tena  nipo kidato cha pili lakini nikawa naendelea  nafanya mazoezi kwa siri.


Atua JKT

Katika harakati za kusaka maisha, alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ambalo lilimfungulia milango ya mchezo wa ngumi.

“Nilipokuwa JKT kuna mwalimu akawa anatafuta wachezaji kambini. Alivyotangaza niliinuka lakini akaniambia sijui nikae chini na yeye akachukua aliona wanafaa kuingia kwenye ngumi.

“Jeshini kuna siku za michezo, nikaomba nicheze nikapewa mtu ambaye alichaguliwa kwenye ile timu ya kwanza na Mungu akajalia nikaweza kumpiga baada ya hapo ndiyo nikaingia kwenye timu,” anasema Waziri.


Aingia ngumi za kulipwa

“Nimeanza kucheza mwaka jana na tofauti yake huku unamjua mpinzani wako mapema tofauti na ngumi za ridhaa na unapata muda wa kuweza kufanya maandalizi makubwa ila ngumi za ridhaa mpinzani unamjua siku ya kupima na hakuna malipo kama kwenye ngumi za kulipwa,” anasema bondia huyo.


Maisha nje ya ulingo

“Baada ya kumaliza muda JKT nimekua nikiendelea na ngumi lakini pia nimekuwa fundi wa kufanya skim kwenye kuta ingawa haina kipato kikubwa kama kwenye ngumi lakini imekuwa ikinisaidia,” anasema Waziri.