IAA, Misitu zaanza vyema nane bora RCL

Muktasari:
- Michuano hiyo ambayo inachezwa na vijana walio chini ya umri wa miaka 20 inashirikisha timu nane ambazo zilishika nafasi mbili za juu katika vituo vinne vya hatua ya awali ambazo zilikuwa Arusha, Mtwara, Kigoma na Shinyanga.
Timu za IAA SC ya Arusha na Misitu ya Tanga zimeanza vyema michuano ya Ligi ya Mabingwa Mikoa (RCL), hatua ya nane bora baada ya kupata ushindi katika mechi za ufunguzi.
Michuano hiyo ambayo inachezwa na vijana walio chini ya umri wa miaka 20 inashirikisha timu nane ambazo zilishika nafasi mbili za juu katika vituo vinne vya hatua ya awali ambazo zilikuwa Arusha, Mtwara, Kigoma na Shinyanga.
Hatua hiyo zinacheza katika makundi mawili yenye timu nne na kila kundi litatoa timu mbili za juu ambazo zitatinga nusu fainali.
Timu mshindi wa nusu fainali itapanda moja kwa moja kucheza First League msimu wa 2025/26, huku mshindi wa tatu na nne zitacheza michezo ya mchujo (playoff) dhidi ya timu za Firt League kwa maana ya timu itakayofungwa kwenye mchujo kati ya Tunduru Korosho dhidi ya Mapinduzi na Copco dhidi ya Magnet.
Leo zimepigwa mechi mbili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Arusha ambapo mchezo wa mapema saa 8:00 ilishhuudiwa Misitu ikionyesha imedhamiria kuitaka First League baada ya kuichapa Igunga United mabao 3-2.
Mabao ya Misitu yalifungwa na Mussa Issa dakika ya 34 kwa penati, Jackson Julias dakika ya 43 na Ramadhani Abedi dakika ya 47.huku mabao ya Igunga yakifungwa na Omary Ismail (aliyejifunga) dakika ya 46 na Hamisi Omari ile ya 61.
Mchezo mwingine ambao ulianza saa 10:00 jioni wenyeji IAA SC imetakata kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bara FC ya Dar Es Salaam.
Mabao ya IAA SC yalifungwa na Abdallah Salum dakika ya 7 na dakika ya Sande Kayanda alitupia katika dakika ya 65.
Ushindi huo unaiweka kileleni IAA SC kwenye msimamo wa kundi A la ligi hiyo kwa alama tatu sawa na Misitu FC huku zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Mechi za kesho Alihamisi zitakuwa za kundi B ambapo mchezo wa kwanza utakaopigwa saa 8:00 mchana itazikutanisha Bandari ya Mtwara dhidi mabao ya Shinyana, huku mchezo wa pili ukitazamiwa kuzikutanisha Kajuna ya Kigoma dhidi ya Cargo ya Dar Es Salaam - mchezo ambao utapigwa kuanzia saa 10:00 jioni.
Makundi ya nane bora RCL kundi A kuna timu za IAAC SC (Arusha), Bara (Dar Es Salaam), Misitu (Tanga) na Igunga (Tabora).
Kundi B lina Kajuna (Kigoma), Cargo (Dar ES Salaam), Bandari SC (Mtwara) na Mabao (Shinyanga).