Prime
Ikanga Speed hakijaeleweka Yanga, azua maswali

Muktasari:
- KABLA ya kutimka kwa aliyekuwa kocha wa Yanga, Sead Ramovic alikuwa alimkalia kooni winga mpya wa timu hiyo, Jonathan Ikangalombo ‘Ikanga Speed’ na kuibua maswali itakuwaje baada ya jamaa kusepa?
KABLA ya kutimka kwa aliyekuwa kocha wa Yanga, Sead Ramovic alikuwa alimkalia kooni winga mpya wa timu hiyo, Jonathan Ikangalombo 'Ikanga Speed' na kuibua maswali itakuwaje baada ya jamaa kusepa?
Hata hivyo, ni kwamba Ikanga Speed amebaki kidogo tu kabla ya kuanz akuliamsha Jangwani kwani baada ya kumaliza programu ya kupunguza uzito, sasa ameanza kuuchezea mpira.
Mwanaspoti imepenyezewa kwamba katika mazoezi ya Yanga, Ikanga Speed anagusa mpira kwa muda mchache sana lakini sehemu kubwa ya mazoezi yake ni kukimbizwa kwa mbio za viwango tofauti baada ya makocha wake kushtukia kitu.
Ikanga Speed hakucheza takribani miezi mitatu wakati akipambana kutaka kusitisha mkataba ili aondoke AS Vita hatua ambayo Ramovic na jopo lake la walimu wa mazoezi hasa wale wa utimamu wa mwili.
Winga huyo alionekana kama ameongezeka uzito kidogo na baada ya hapo alipewa kocha wa utimamu wa mwili ambaye ndiye anayepambana naye kumweka sawa, huko kwenye Uwanja wa mazoezi.
Hata hivyo, wiki hii winga huyo aliaanza kupewa muda mchache wa kucheza mpira ambapo akaanza kuonyesha ubora wake akijua kuwakimbiza mabeki na kupambana na nguvu huku pia akiwa na kasi ya kuelekea langoni.
Mapema siku moja kabla ya Ramovic kuachia ngazi kocha huyo akizungumzia Ikanga Speed akisema winga huyo bado anaendelea kuandaliwa ili kuepusha asiumie endapo atawahishwa kucheza kwenye kikosi hicho.
"Jonathan (Ikangalombo) ni mchezaji mzuri, jambo la kwanza tunalopaswa kufanya, bila shaka ni kumfikisha katika kiwango cha utimamu wa mwili tunachotaka kwa sababu si tu kuhusu utimamu wake wa mwili bali pia kuhakikisha kwamba hapati majeraha," alisema Ramovic na kuongeza;
"Ikiwa Hana kiwango sahihi cha utimamu wa mwili na anahitaji kukimbia kwa kasi kwenye mechi, Kuna uwezekano mkubwa wa kuumia na hilo ndio tunalotaka kupika."
Winga huyo amezua taharuki ambapo tangu asajiliwe dirisha dogo hajaonekana kwenye mechi yoyote zaidi ya kuwa juu ya jukwaa hatua ambayo mashabiki wa Yanga walianza kupata wasiwasi.
Hata hivyo, winga huyo bado anaonekana atapita njia hiyo hiyo chini ya kocha mpya wa Yanga Miloud Hamdi ambaye naye ni muumini mzuri wa utimamu wa kiwango kikubwa wa mwili.