Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jina la straika Mchad latua Simba

STRAIKA Pict


WEKUNDU wa Msimbazi, Simba wameanza kimyakimya mchakato wa kuiboresha safu yao ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao huku jina la mshambuliaji mahiri wa Golden Arrows, raia wa Chad, Junior Dion, likitajwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa.


Taarifa zilizopo zinaeleza uongozi wa Simba, kwa kushirikiana na benchi la ufundi, unaona wazi haja ya kuongeza nguvu mpya eneo la ushambuliaji, hasa baada ya timu hiyo kuonyesha mapungufu ya wazi licha ya maboresho yaliyofanywa dirisha la usajili la Januari.


Dion ambaye anang’ara katika Ligi ya Afrika Kusini, amekuwa katika kiwango bora. Hadi sasa, amefunga mabao 13 na kutoa asisti moja katika mechi 24 za ligi, rekodi inayomfanya kuwa miongoni mwa washambuliaji hatari zaidi kwa sasa nchini humo.

STRA 01

Inaelezwa kuwa kocha wa Simba, Steve Barker, tayari amewasilisha mapendekezo ya majina matatu ya washambuliaji anaotaka kusajiliwa huku Dion akitajwa kuwa chaguo muhimu katika mpango huo.

Hata hivyo, dili lake halitakuwa rahisi, kwani thamani yake inatajwa kufikia zaidi ya Dola 240,000 (ni zaidi ya Sh630 milioni).

Kwa sasa, safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na Seleman Mwalimu ambaye ameifungia timu hiyo mabao sita pekee katika ligi, jambo linaloongeza presha ya kutafuta mshambuliaji mwingine ambaye anaweza kuongeza nguvu eneo hilo, ikumbukwe kuwa Mwalimu naye yupo Msimbazi kwa mkopo akitokea Wydad Casablanca ya Morocco na mwishoni mwa msimu atarejea kwenye timu yake.

STRA 02

Hali ilizidi kuwa tofauti kwa Simba katika safu yao ya ushambuliaji baada ya kusimamishwa kwa Jonathan Sowah kutokana na masuala ya kinidhamu.

Kabla ya tukio hilo, Sowah alikuwa mmoja wa washambuliaji muhimu kwenye kikosi hicho lakini sasa dalili zinaonyesha huenda akaachana na miamba hiyo. Hii ni licha ya rekodi yake nzuri msimu uliopita alipokuwa akiichezea Singida Black Stars na alifunga mabao 13 na kuwa mmoja wa washambuliaji hatari.

Kwa upande wa Dion, safari yake ya soka la kulipwa imekuwa ya kupanda hatua kwa hatua. Aliingia katika ramani ya soka la Afrika Kusini mwaka 2021 alipojiunga na Marumo Gallants akitokea Jwaneng Galaxy.

Baadaye alihamia AmaZulu FC kabla ya kutua Golden Arrows ambapo sasa anafurahia msimu wake bora zaidi kuwahi kutokea.

Katika mashindano yote msimu huu, Dion amecheza michezo 30, akifunga mabao 14 na kutoa asisti mbili ndani ya dakika 2,316. Tofauti na msimu uliopita wa 2024/25 alipokuwa AmaZulu na alifunga mabao matatu katika mechi 20.

STRA 03

Dion si mgeni kwa kocha Barker, wawili hao waliwahi kukutana wakati Barker akiinoa Stellenbosch FC na Dion alicheza dhidi yake katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Carling Knockout Cup.

Katika mchezo huo, alicheza kwa dakika 63 na kuonyesha kiwango kizuri licha ya kutofunga huku Stellenbosch ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1.


Wasifu wa Junior Dion

Kuzaliwa: Oktoba 15, 1998 (miaka 27)

Mahali: Abidjan, Ivory Coast

Uraia: Chad

Urefu: Mita 1.82

Nafasi: Mshambuliaji wa kati