Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Karibu Ibenge tutakupima kimataifa

Muktasari:

  • Baada ya kuiongoza Azam kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi, kocha mwandamizi Rachid Taoussi atapewa mkono wa kwaheri kumpisha Ibenge anayetokea Al Hilal ya Sudan.

MATAJIRI wa Azam FC wamecharuka kweli na kijiweni hapa tumepata habari za uhakika kutika viunga vya Azam Complex kule Chamazi kuwa kocha mpya ajaye ni Mkongomani Florent Ibenge.

Baada ya kuiongoza Azam kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi, kocha mwandamizi Rachid Taoussi atapewa mkono wa kwaheri kumpisha Ibenge anayetokea Al Hilal ya Sudan.

Hapana shaka, Taoussi ni kocha mkubwa na mzuri, lakini namba za msimu huu zimemuangusha sasa kiuhalisia ingekuwa ngumu kwake kubaki kwa watengeneza Aiskrimu.

Taoussi aliikuta Azam iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu wa 2023/2024 lakini chini yake imemaliza ya tatu na pia katika Kombe la TFF, Azam katika msimu huu imetolewa katika hatua ya 16 bora wakati msimu mmoja kabla ilifika fainali.

Sasa anakuja Ibenge. Kocha mkubwa sana Afrika na iko wazi ana heshima iliyoje kutokana na makubwa aliyofanya kwenye timu alizowahi kuzifundisha kwa nyakati na mechi tofauti.

Kitendo cha kumchukua Ibenge kinatupa picha kwamba sasa Azam wanataka kuona timu yao inapata mafanikio makubwa hasa katika mashindano ya kimataifa kwa vile Ibenge ni kocha wa hadhi hiyo. Huwezi kulipa mafedha mengi Ibenge ili ashindanie taji na kina Mbeya City au KMC.

Na kumekuwa na mitazamo kwamba katika mashindano ya ndani hapa Tanzania, Azam haifanyi vizuri kwa vile imewekwa mtu kati na Yanga na Simba ambazo haziipi nafasi ya kuchomoza katikati yao na kutamba katika vita ya kuwania makombe ya ndani.

Sasa basi kwa vile Simba na Yanga ndio kikwazo kikubwa cha Azam hapa ndani, basi tunategemea chini ya Ibenge itatikisa kimataifa kwani huko hakuna mbambamba na hao ambao wanatajwa kuwa wanaiwekea kauzibe hapa ndani.

Kombe la Shirikisho Afrika ni saizi kabisa ya Ibenge na Azam kufanya vizuri hivyo tunaweza kusema upele umepata mkunaji.