Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kibadeni: Singano ameiva

Ramadhan Singano

Muktasari:

“Alipotua Azam, hakufanikiwa kuonekana mapema, ila ni mchezaji mzuri anajua kufunga, kutoa pasi, kupiga kona, kutoa mashambulizi ya kulia na kushoto, kilichobaki sasa ni kwa kocha wake kumjenga ili ajitambue na kuwa na mtazamo wa mbali,” alisema.

KAZI kubwa aliyoionyesha Ramadhani Singano wa Azam katika mchezo wa kimataifa dhidi ya Esperance ya Tunisia, imemfanya kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni kushindwa kuvumilia na kutamka kuwa, ‘huyu dogo kaiva kwelikweli’.

“Alipotua Azam, hakufanikiwa kuonekana mapema, ila ni mchezaji mzuri anajua kufunga, kutoa pasi, kupiga kona, kutoa mashambulizi ya kulia na kushoto, kilichobaki sasa ni kwa kocha wake kumjenga ili ajitambue na kuwa na mtazamo wa mbali,” alisema.

Kibadeni alisema njia ni wazi kwa Singano kucheza soka la kulipwa kwa sababu ana nidhamu na pia ni mcha Mungu, hilo linambeba kulinda kiwango chake kuwa juu kwa muda mrefu.

“Nilianza kumfundisha tangu alipokuwa Kikosi B na Simba A, anajielewa na alikuwa anapenda kujua vitu vya kiufundi, Azam ni timu iliyojitosheleza kwa mahitaji ya wachezaji, asibweteke avitumie kwa manufaa ya kuwa wa kimataifa,” alisema.

Alisema kwa sasa Singano anatakiwa apiganie kujumuishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho kitazidi kumtambulisha kwenye mataifa mbalimbali kama alivyoonyesha uwezo walipocheza na klabu ya Esperance.

“Umri wake unamruhusu kucheza nje, aangalie Mbwana Samatta alipo, akijitambua, akijua wa kimataifa wanahitaji wa aina gani, akifuata maelekezo ya kocha wake Stewart Hall, atakuwa faida kwa taifa kama walivyo Samatta na Thomas Ulimwengu.”