Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiut bingwa Provincal CUP

Provocal Pict

Muktasari:

  • Mashindano hayo ya kombe la Provincial yaliandaliwa na kituo cha Donbosco, Oyster bay, yakishirikisha DB VTC, Don Rua, IFM, Kigamboni Academy, DB Oratory, MUHAS  na KIUT.

KIUT imedhihirisha ubora wake baada ya kuifunga DB Oratory  kwa pointi 72-54 katika fainali ya kombe la Provincial kwenye Uwanja wa Donbosco, Oysterbay.

Mashindano hayo ya kombe la Provincial yaliandaliwa na kituo cha Donbosco, Oyster bay, yakishirikisha DB VTC, Don Rua, IFM, Kigamboni Academy, DB Oratory, MUHAS  na KIUT.

Katika mchezo huo, KIUT ilidhibiti eneo lote la uwanja, hali iliyofanya DB Oratory kupoteana na kuchapwa katika robo zote nne kwa pointi 20-13, 15-12, 14- 12 na 23-17.

Samson Mabula wa KIUT aliongoza kwa kufunga pointi 28, huku akifunga tisa kwa mitupo ya pointi tatu na asisti saba, akifuatiwa na Douglas Mollel aliyefunga 19, huku Dominic Kipingu wa DB Oratory akifunga 12.

Kocha wa KIUT, Denis Funganoti alipongeza timu zote kwa ushindani mkubwa walionyesha kwa siku zote.

“Timu zilipambana kwa kweli na ushindi wetu ulichangiwa na maandalizi tuliyokuwa tunafanya katika uwanja wa KIUT,” aliema Funganoti.

Alisema mashindano hayo pia ni moja ya maandalizi yao ya ligi ya kikapu Mkoa wa Dar es Salaam BDL mwaka huu na yanaenda vizuri.