Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha JKT ataka rekodi mpya Isamuhyo

JKT Pict

Muktasari:

  • JKT itaipokea Simba ikiwa ndio kwanza imetoka kuing’oa Stellenbosch ya Afrika Kusini kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo katika kiporo cha Ligi Kuu Bara, huku kocha Hamad alisema anataka kuendelea kulinda rekodi ya uwanja huo kwa kutofungwa nyumbani.

LICHA ya Simba kutinga fainali Kombe la Shirikisho Afrika baada ya miaka 32 tangu ilipofanya hivyo kwa kucheza fainali ya Kombe la CAF 1993, lakini hilo wala halijamtisha Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Hamad Ally aliyetamba mechi dhidi ya mnyama anataka rekodi mpya ikiwa nyumbani.

JKT itaipokea Simba ikiwa ndio kwanza imetoka kuing’oa Stellenbosch ya Afrika Kusini kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo katika kiporo cha Ligi Kuu Bara, huku kocha Hamad alisema anataka kuendelea kulinda rekodi ya uwanja huo kwa kutofungwa nyumbani.

JKT Tanzania imepoteza mechi moja tu msimu huu ikiwa nyumbani dhidi ya Singida BS kwa bao la Jonathan Sowah, huku timu nyingine zikichezea vichapo vya kizalendo au kuambulia sare, ikiwamo Yanga iliyoambulia suluhu na Kocha Hamad alisema hata kwa Simba wasitarajie mteremko Mei 2.

Akizungumza na Mwanaspoti, Hamad alisema wanaheshimu ubora wa Simba lakini ni timu ambayo wamekuwa wakicheza nayo mechi za ligi, hivyo mambo ya kimataifa wao wanayaweka pembeni na kuangalia dakika 90 zilizo mbele yao kuhakikisha wanalinda mwiko kupoteza wakiwa nyumbani.

“Ni kweli tunakutana na timu ambayo imetoka kufanya vizuri kimataifa tunaheshimu walichokifanya na sisi tumejiandaa kuhakikisha tunaweka rekodi ya kuifunga timu iliyotoka kufanya vizuiri kimataifa tukiwa uwanja wetu wa nyumbani tutaingia kwa kuwaheshimu,” alisema Hamad na kuongeza;

“Kikosi changu kinaendelea vizuri na maandalizi na tunatambua ubora uliopo dhidi ya mpinzani wetu hilo halitufanyi tukaingia na ubaridi tupo vizuri na wachezaji wanatambua ugumu wa mchezo ulio mbele yetu tunasahihishana makosa na kuboresha maeneo ambayo tunaamini wapinzani wetu ni bora ili tuwe kwenye nafasi nzuri ya kuwadhibiti.”

Alisema wachezaji wa JKT wanatakiwa kuwa bora kwa kila tukio kiwanjani kwani wanaenda kukutana na timu ngumu na bora kwenye ligi kuokana na kuwa kwenye kilele cha mafanikio na wanasaka nafasi ya uwakilishi kimataifa.

JKT ilikuwa inashikilia rekodi bora ya timu ambazo hazijapoteza zikiwa nyumbani kwani kabla ya mchezo na Singida Black Stars, timu hiyo ilikuwa imecheza michezo tisa ya mashindano yote na kati yake minane ni ya Ligi Kuu Bara na mmoja wa Kombe la FA.

JKT itaingia katika mchezo huu ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza wakikubali kichapo cha bao 1-0 bao la mkwaju wa penati uliochongwa na  Charles Ahoua dakika za jioni.