Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Licha ya mvua, mamia wajitokeza kuuaga mwili wa Charles Hilary

Muktasari:

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar, Charles Hilary alifariki dunia alfajiri ya Mei 11 katika Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Licha ya mvua kubwa kunyesha katika mji Unguja, Zanzibar wananchi na viongozi kutoka maeneo mbalimbali wamefika Kisonge kwa ajili ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Charles Hilary, ambapo zoezi hilo litaongozwa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar, Charles Hilary alifariki dunia alfajiri ya Mei 11 katika Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu

Charles kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo Desemba 30, 2021, kisha kuteuliwa kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Februari 6, 2023 alikuwa mtangazaji wa vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania.

Mkurugenzi huyo, amewahi kufanya kazi katika vituo mbalimbali ndai na nje ya nchi ikiwamo Redio Tanzania kwa sasa TBC Taifa, Redio One, Sauti ya Ujerumani (DW), Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na Azam alikokuwa wakati akiteuliwa kwenda katika majukumu ya ukurugenzi wa Rais, Ikulu Zanzibar hadi mauti yanamkuta.

Mwili wa Charles Hilary uliwasili jana Jumanne kupitia Bandari ya Malindi kwa ajili ya kuagwa.

Charles alikuwa ni mtoto wa pili wa familia ya Martin Hilary, akiwa amezaliwa Oktoba 22, 1959 katika Mtaa wa Jang'ombe na kukulia Makadara mjini Unguja visiwani hapa.

Wananchi waliofika katika maeneo hayo wamesema watamkumbuka kiongozi huyo kwa ucheshi aliokuwa nao, kwani licha ya kuwa na nyadhifa kubwa serikali lakini bado alikuwa na upendo kwa kila mmoja.

Mohammed Mussa, amesema amefika kuuaga mwili wa Charles kwa sababu ameguswa na kifo chake kutokana na upendo aliokuwa nao hivyo ameona haitokuwa vizuri kama hatofika eneo hilo.

Naye Kulpara Ahmed (Dj Kulpara) amesema marehemu alikuwa mtu wake wa karibu sana na leo amevaa fulana na kofia aliyomletea zawadi wakati akitoka Cuba ikiwa ni sehemu ya kumuenzi.

"Charles aliniletea zawadi hii, akaniambia wakati wowote nitakapoivaa nitamkumbuka na ndio maana nimevaa kwa ajili ya kumuenzi," amesema Kulpara.

Wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari wameshawasili Kisonge kwa ajili ya kuaga mwili huo wakiwamo, Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Gerson Msigwa, mtangazaji wa Wasafi Radio, Maulidi Kitenge na viongozi wa vyombo mbali mbali vya habari kama Azam Media, Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).