Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Shangwe zateka msafara wa Simba, yatua Morocco

Muktasari:

  • Ni safari iliyochukua saa 8:40 angani, lakini kwa mashabiki wa Simba ilikuwa ni fupi kutokana na shangwe ambazo walikuwa nazo kuanzia mwanzo wa safari hadi tulipotua hapa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mohamed V.

Simba imewasili Casablanca, Morocco alfajiri ya leo  saa 10:20 hapa ikiwa ni saa 1:20 kwa saa za Tanzania.

Ni safari iliyochukua saa 8:40 angani, lakini kwa mashabiki wa Simba ilikuwa ni fupi kutokana na shangwe ambazo walikuwa nazo kuanzia mwanzo wa safari hadi tulipotua hapa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mohamed V.

Ndani ya ndege ya Shirika la Ndege la Air Tanzania, mashabiki wa Simba walikuwa wamewasha muziki katika redio ambayo mmoja wao amesafiri nayo na wakawa wanacheza.

Jumamosi, Mei 17, 2025 Simba itacheza mechi ya kwanza ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane.

Simba imetinga hatua hiyo kwa mara ya kwanza tangu michuano hiyo ilipoasisiwa mwaka 2004 kwa kuunganishaa kwa Kombe la Caf na Kombe la Washindi Afrika, baada ya kuing'oa Stellenbosch ya Afrika Kusini.

Hata hivyo, Simba ilishacheza fainali ya Kombe la CAF 1993 na kupoteza kwa mabao 2-0 mbele ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.