Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mangungu, Hersi bungeni wasitusahau

Muktasari:

  • Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu na Rais wa klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said.

KUNA roho fulani inaniambia kuwa viongozi wawili wa juu wa klabu za Simba na Yanga watajitosa kuwania ubunge katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu na Rais wa klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said.

Kwa namna ambavyo hawa watu wamepata mafanikio katika uongozi wa klabu hizo mbili, karoho kananiambia kwamba watachukua fomu za kuwania ubunge siku sio nyingi zijazo.

Roho inaniambia kuwa Mzee wangu Murtaza Mangungu ataomba ridhaa kule Kilwa ambako anapataja kuwa sehemu bora zaidi katika maisha yake na Mhandisi Hersi Said nafsi inanishawishi kuwa ataomba kuliongoza jimbo mojawapo hapa Dar es Salaam.

Kama wawili hao watafanya hivyo kama ambavyo karoho fulani kamenishawishi itakuwa jambo la kheri sana kwa vile wananchi wa majimbo hayo watakuwa wamepata watu makini na wenye uwezo mzuri wa kiuongozi.

Hata hivyo, ombi la kijiwe kwao iwapo wataona haja ya kuwania ubunge, basi ikitokea wameupata watukumbuke watu wa soka na wakiingia katika muhimili huo mmojawapo wa nchi basi wapiganie sana maslahi ya mchezo huo pendwa.

Katika uongozi wao wa Yanga na Simba wanakutana na kuziona changamoto nyingi zinazotakiwa kufanyiwa kazi hivyo kutumia uzoefu wao kwenda kuzisemea Bungeni litakuwa jambo lenye manufaa makubwa kwa mchezo wa mpira wa miguu.

Na wao wakipita kisha wakapata fursa ya kuusemea mchezo wa soka, mambo yatakuwa rahisi kufanyiwa kazi kwa vile watu wataamini yanatoka kwa wanaoufahamu uhalisia wa maisha ya soka nchini mwetu.

Sio tena wakifika huko wanatusahau wanafamilia wenzao wa mpira wa miguu na kushindwa kutusaidia kutufikishia au kupeleka changamoto zinazotukabili wakati wao wana uzoefu nazo.