Mchezaji wa Utah Jazz apata corona, NBA yasimamisha mechi zote

Muktasari:
Nyota huyo wa NBA aliyegundulika na corona hakuwepo katika mchezo huo
Oklahoma, Marekani. NBA imetangaza mechi zote za ligi hiyo zimesimamishwa kuanzia leo Alhamisi hadi hapo itakapotangazwa tena baada ya mchezji wa Utah Jazz kubainina na dalili za ugonjwa wa Corona.
Tangazo hili lilitolewa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Utah Jazz dhidi ya Oklahoma Thunder jana Jumatano.
Nyota huyo wa NBA aliyegundulika na corona hakuwepo katika mchezo huo.
"NBA imeamua kuchukua hatua stahiki za tahadhali juu ya janga la ugonjwa wa corona," ilisema taarifa hiyo.
The Jazz v Thunder imehairishwa.
Taarifa ambayo siyo rasmi inasema mchezaji aliyepata ugonjwa huo ni Rudy Gobert.
Utah Jazz ilisema mchezaji huyo awali hakuonekana na tatizo, lakini baadaye alibainika kuwa visusi Covid-19, vinavyosababisha corona.