Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlandege yaizima Mwembe Makumbi Ligi Kuu Zanzibar

MWEMBE Pict

Muktasari:

  • Dakika 90 za mchezo wa wababe wa ligi hiyo M/Makumbi na Mlandege imemalizika kwa ushindi wa bao 2-0 kwenye Uwanja wa Mao A, Mjini Unguja.

VINARA wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), Mwembe Makumbi imekumbana na kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mlandege katika pambano kali lililopigwa kwenye Uwanja wa Mao A, mjini Unguja.

Katika pambano la duru la kwanza  timu hizo zilishindwa kutambiana kwa kufungana mabao 2-2 kwenye Uwanja wa New Amaan na leo ikiwa moja ya mechi za raundi ya 23  Mlandege ikafanya kweli kwa ushindi huo. 

Katika mechi ya leo, Mlandege iliandika bao la kwanza dakika ya 11 kupitia kwa Abdallah Idd lililodumu hadi mapumziko.

Bao la pili la Mlandege lilifungwa dakika ya 50  likiwekwa pia na Abdallah Idd na kuifanya timu hiyo ifikishe pointi 44, moja pungufu na ilizonazo Mwembe Makumbi inayoongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na 45 kila moja ikicheza mechi 23.

Katika mchezo mwingine uliopigwa kisiwani Pemba kwenye  Uwanja wa Finya, Chipukizi na Mwenge zilishindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu.

Ligi hiyo itaendelea kesho Jumapili kwa Malindi kuumana na KMKM kwenye Uwanja wa Mao A, ilihi Kipanga itacheza na Mafunzo.