Mtanzania anyakua ndoo Misri

Muktasari:
- Huu ni msimu wa pili mfululizo kwa Ubamba kuitumikia klabu hiyo akisajiliwa kwa mkopo kutokea Fountain Gate Princess ya Tanzania.
WINGA wa FC Macar, Mtanzania Hasnath Ubamba amebeba ubingwa wa Ligi ya Wanawake nchini Misri ukiwa wa pili mfululizo kwa nyota huyo.
Huu ni msimu wa pili mfululizo kwa Ubamba kuitumikia klabu hiyo akisajiliwa kwa mkopo kutokea Fountain Gate Princess ya Tanzania.
Msimu wa kwanza alifanikiwa kunyakua taji la ligi na kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake, timu hiyo ikimaliza nafasi ya tatu.
Msimu huu tayari chama hilo limenyakua ubingwa kwa kuifunga Zamalek bao 1-0 na ina mchezo mmoja mkononi wa kumalizia ratiba.
Macar imecheza mechi 16 ikikusanya pointi 46, ikishinda mechi 15 na sare moja.