Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwamnyeto: Kwa usajili huu, mtusamehe tu yaani

Muktasari:

NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ameiambia Mwanaspoti kwamba kama kuna wakati Yanga imesajili timu bora basi ni sasa.

NAHODHA wa Yanga, Bakari Mwamnyeto ameiambia Mwanaspoti kwamba kama kuna wakati Yanga imesajili timu bora basi ni sasa.

Mwamnyeto ambaye sio mtu wa kuongea sana alisema karibu idara zote zimesajiliwa vyema wakiongezwa watu hasa waliostahili kuingia wakiwa na ubora mkubwa.

“Huu usajili uliofanyika safari hii ni kama funga kazi, hakuna tena timu ya kutufanya tukose mataji, huu ndio wakati ambao viongozi wamesajili watu wa kweli hasa,” alisema Mwamnyeto ambaye ni mchezaji wa zamani wa Coastal Union.

“Ukiangalia kila eneo kumeletwa watu hasa, washambuliaji waliokuja ni wazuri sana, viungo wa pembeni nao ni wakali ukiongeza na wale wa kati, haya huku kwenye ulinzi nako kuna watu wa maana,” alisema.

Aliongeza, hata kama kuna timu zitakuwa zimejiandaa vyema lakini msimu ujao kwa timu waliyonayo hakuna sababu ya wao kukosa mataji na kwamba kwasasa wanajipanga vyema ili wawe tayari kwa ushindani.

“Najua kila timu inajipanga sawa, lakini huku kwetu tuko sawasawa kuhakikisha mataji tunayachukua msimu ujao.”