Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namungo yapangwa kundi la kifo Shirikisho

Muktasari:

  • Namungo inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote katika mechi ya marudiano na De Agosto ili itinge hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika


Wakati ikionekana ina nafasi kubwa ya kutinga hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika, Namungo FC itaangukia kundi D la mashindano hayo ikiwa itaitupa nje Primiero De Agosto ya Angola.

Katika droo ya hatua ya makundi ya mashindano hayo iliyochezeshwa leo huko Cairo, Misri, Namungo wamepangwa katika kundi hilo linaloonekana kuwa la kifo sambamba na timu za Nkana (Zambia), Raja Casablanca (Morocco) na Pyramids (Misri).

Raja Casablanca ni mabingwa wa taji la mshindano hayo mwaka 2018 lakini pia wamewahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mara tatu ambazo ni 1989, 1997 na 1999.

Pyramids FC wenyewe msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya pili ya mashindano hayo baada ya kufungwa na RS Berkane katika fainali.

Mafanikio makubwa kwa Nkana FC yalikuwa ni kutinga hatua ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 1990 wakati Namungo FC ndio wanashiriki kwa mara ya kwanza.

Namungo FC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-2 katika mechi ya kwanza jana dhidi ya Agosto, inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote iweze kutinga kwenye makundi.

Kundi A la mashindano hayo lina timu za Enyimba (Nigeria), ES Sétif (Algeria),
Orlando Pirates (Afrika Kusini) na  Ahli Benghazi (Libya) wakati kundi B lina timu za RS Berkane (Morocco), JS Kabylie (Algeria), Cotonsport (Cameroon) na NAPSA Stars (Zambia)

Nalo kundi  C litakuwa na timu za Etoile Sahel (Tunisia),
CS Sfaxien (Tunisia),  Salitas (Burkina Faso) na ASC Jaraaf (Senegal)