Ngai: Simba inatuhujumu mapato

Muktasari:
- Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Alexander Ngai akisema anaunga mkono msimamo wa klabu yake kwamba timu yao itaenda uwanjani kwa ajili ya mchezo huo.
Yanga imesisitiza kwamba haitakubali mchezo wa Dabi ya Kariakoo uliopangwa leo uahirishwe huku ikisema watani wao Simba wanaihujumu mechi hiyo ili kuwanyima mapYanga imesisitiza kwamba haitakubali mchezo wa Dabi ya Kariakoo uliopangwa leo uahirishwe huku ikisema watani wao Simba wanaihujumu mechi hiyo ili kuwanyima mapato.ato.
Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Alexander Ngai akisema anaunga mkono msimamo wa klabu yake kwamba timu yao itaenda uwanjani kwa ajili ya mchezo huo.
Ngai amesema Simba ambayo imetoa tamko kwamba haitaleta timu uwanjani, inafanya uamuzi huo ikiwa na hesabu za kuwakwamisha kimapato ya mchezo.
"Kwanza naungana na msimamo wa klabu kwamba sisi Yanga tutapeleka timu uwanjani kama ambavyo ilikuwa kabla, wao walete timu tucheze mechi tumalizane," amesema Ngai.
"Simba wanafanya haya kwa makusudi kutukwamisha Yanga kupata mapato kwa kuwa wanajua kwamba mchezo wa kwanza walipata fedha na safari hii zamu yetu kupata fedha, Bodi ya Ligi na TFF waliangalie hili."
Aidha, Ngai ameongeza kuwa bado hajaona sababu kubwa ya Simba kufanya uamuzi kama huo, ambapo Yanga itapeleka timu uwanjani mapema tu kuwasubiri watani wao hao.
"Timu yetu itawahi mapema tu uwanjani, tutafuata taratibu zote za kimchezo, kitu muhimu ni kwamba tuna kikosi chenye wachezaji wakomavu, hawajaathirika na lolote wanasubiri mchezo husika."