Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni Mwamnyeto na Yondani Stars

New Content Item (1)
v

Muktasari:

KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameonekana kutengeneza ukuta wa timu yake kwa kuwapanga mabeki visiki Bakary Mwamnyeto na Kelvin Yondani kuelekea mechi ya kirafiki na Kenya jijini Nairobi, Jumatatu.

KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameonekana kutengeneza ukuta wa timu yake kwa kuwapanga mabeki visiki Bakary Mwamnyeto na Kelvin Yondani kuelekea mechi ya kirafiki na Kenya jijini Nairobi, Jumatatu.

Katika mazoezi ya Jumanne jioni kocha Kim aliwapanga Juma Kaseja, Hassan Kessy, Bakari Mwamnyeto, Kelvin Yondani, Bryson Rafael, Edward Charles, Ayoub Lyanga, Baraka Majogoro, Nassor Saadun, Abdul Suleiman na Deus Kaseke.

Timu nyingine ikiwa na Metacha Mnata, Israel Patrick, Yassin Mustapha, Dickson Job, Laurent Alfred, Feisal Salum, Idd Seleman, Salum Abubakari, Kelvin John, Farid Mussa na Meshack Abraham. Kocha huyo alikuwa akiangalia namna ambavyo mfumo wake unavyofanya kazi wakitumia mfumo wa 4-4-2 na akitaka wacheze soka la utulivu na umakini kwa upande wa viungo na washambuliaji kwenye kushambulia.

Pia, Kim alikuwa anawataka mabeki hasa Mwamnyeto na Yondani wawe makini katika ukabaji na kazi hiyo walifanya kwa ufasaha jambo ambalo Kim lilionekana muda wote kumpa tabasamu.

Katika mazoezi ya jana Jumatano asubuhi, Kim hakubadilisha sana kikosi na aina ya mazoezi waliyofanya siku ya kwanza, kwani aliwapanga Juma Kaseja, Israel Patrick, Yassin Mustafa, Bakari Mwamnyeto, Kelvin Yondani, Baraka Majogoro, Ayoub Lyanga, Feisal Salum, Nassor Saadun, Abdul Suleiman na Deus Kaseke. Kikosi kingine kilikuwa na Metacha Mnata, Hassan Kessy, Edward Charles, Dickson Job, Laurent Alfred, Salum Abubakari, Deus Kaseke, Farid Mussa na Meshack Abraham.