Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nidhamu yambeba Mandonga

NIDHAMU imetajwa kumbeba bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini,  Karim Said “Mandonga mtu kazi” ambaye ameingia mkataba usio na kikomo.

Mkataba huo ni wa ubalozi wa Kampuni ya Mr. Discount Hyper and Supermarket Limited na duka la viatu la Relaxo.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Khalid Mbarak Salim alisema wameingia ‘dili’ hilo na Mandonga kutokana na nidhamu aliyonayo kwenye mchezo wa ngumi na kuwavutia mashabiki wengi.

Salim alisema wamefurahishwa sana na uwajibikaji wa Mandonga tangu aanze kushiriki katika ngumi za kulipwa na amekuwa akijihimarisha na kuwa bondia maarufu zaidi nchini katika mchezo huo.

Alisema haikuwa kazi kubwa kwao kumchagua Mandonga kuwa balozi wa maduka na bidhaa zao na kuingia naye mkataba usiokuwa na kikomo.

“Ni bondia mwenye nidhamu ya hali ya juu katika ngumi za kulipwa, tumependa utendaji wake na hii ndiyo sababu kubwa ya kuingia naye mkataba kuwa balozi wetu,” alisema Salim.

Alisema watapanua wigo wa ubalozi wa bidhaa za na sasa wanatafuta mchezaji wa mpira wa miguu na riadha.

Kwa upande wake, Mandonga alisema amefuraishwa na makubaliano na kampuni hiyo kupitia mkurugenzi mtendaji wake, Salim na kuahidi kufanya kazi hiyo kwa bidi na uadilifu mkubwa.

“Haya ni matunda ya kujituma na nidhamu kazini. Hii ni faraja kwangu, naahidi kufanya vyema zaidi,” alisema Mandonga.

Alisema mabondia wanatakiwa kujitafakari na kuendesha michezo hiyo katika hali ya nidhamu ili makampuni  mbalimbali yavutiwe na kuingia mikataba ya ubalozi kama ilivyokuwa kwake.