Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pacome ampa mzuka Hamdi

Muktasari:

  • Mastaa hao waliumia kwa nyakati tofauti, huku Aucho akipata jeraha la kuchanika misuli ya paja, ilhali Pacome aliumia katika mechi dhidi ya Azam na Musonda akiumia kwenye pambano la kwanza la Kombe la Muungano ambako Yanga ilibeba ubingwa.

ALIANZA kurejea Khalid Aucho, lakini kambini Yanga mzuka umeongezeka baada ya nyota wengine wawili waliokuwa majeruhi, kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua na straika Kennedy Musonda kurejea mazoezini, jambo lililomfurahisha kocha Miloud Hamdi.

Mastaa hao waliumia kwa nyakati tofauti, huku Aucho akipata jeraha la kuchanika misuli ya paja, ilhali Pacome aliumia katika mechi dhidi ya Azam na Musonda akiumia kwenye pambano la kwanza la Kombe la Muungano ambako Yanga ilibeba ubingwa.

Wachezaji hao tayari wameungana na wenzao wanaojiandaa kwa mechi za kufungia msimu Ligi Kuu Bara na nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Akizungumza na Mwanaspoti, Hamdi alisema wamepata nguvu zaidi kuwaona wachezaji hao tena mazoezini.

Alisema uwepo wao ni kama kurejea kwa silaha ambazo zilikosekana kwa katika mechi zilizopita. Lakini, pamoja na kukosekana kwao Yanga haijapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya kubeba pointi tatu.

“Nafurahia kuwa na kikosi imara ambacho kinanipa nguvu ya kufanya mzunguko navyotaka kulingana na wapinzani watakavyokuja,” alisema Hamdi

Yanga ambayo iko kileleni katika msimamo wa ligi imecheza mechi 26 na kuvuna pointi 70, ikishinda 23, sare moja na kupoteza miwili.

Timu hiyo itashuka kwenye mchezo wa 27 dhidi ya Namugo, Mei 13 ikiwa nyumbani ambapo katika mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo iliifunga mabao 2-0 ugenini.