Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pamba Jiji yaziendea msituni pointi sita

PAMBA Pict

Muktasari:

  • Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya kupita takribani miaka 23, Jumatatu wiki hii imeondolewa kwenye Kombe la FA kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania.

PAMBA Jiji imekubaliana na kipigo ilichokipata katika robo fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), lakini imesema haitakubali kuona inashindwa kupata pointi sita katika mechi mbili zijazo katika Ligi Kuu Bara ili kuwa sehemu salama zaidi.

Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya kupita takribani miaka 23, Jumatatu wiki hii imeondolewa kwenye Kombe la FA kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania.

Kikosi hicho kinachoshika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi, kimecheza mechi 26 na kushinda sita tu, sare zikiwa tisa na kupoteza 11, hivyo ina pointi 27.

Kwa sasa Pamba Jiji inapiga hesabu za pointi sita za ugenini kabla ya kurudi nyumbani kuzisaka zingine katika mechi nne zilizobaki ili kupata nafasi nyingine ya kuendelea kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Kocha wa Pamba Jiji, Fred Felix ‘Minziro’ aliliambia Mwanaspoti kwa sasa wanaelekeza akili na nguvu zao kujiandaa na mechi hizo dhidi ya Simba (Mei 8), kisha KenGold (Mei 13), zote za ugenini.

Minziro alisema kwenye mechi hizo hawatakwenda kinyonge na wanataka kuhakikisha wanavuna pointi sita za ugenini zitakazowapa nafasi kubwa ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

“Tunaingia kambini kujiandaa na mechi hizo mbili za kwanza za ugenini, tutaanza na Simba kisha baadaye tutawafuata KenGold,” amesema Minziro na kuongeza.

“Tunahitaji pointi zisizopungua sita katika mechi mbili za kwanza kabla ya kurudi nyumbani, ili tuwe na uhakika wa kubaki kwenye ligi, tutazitafuta na tutazipata kwenye mechi hizi zilizosalia.”

Ukiacha mchezo wa ugenini dhidi ya Simba utakaopigwa Mei 8, kisha ule wa KenGold Mei 13, Pamba Jiji itarudi nyumbani kumalizana na JKT Tanzania (Mei 21) kisha kufunga msimu na KMC (Mei 25).

Takwimu zinaonesha Pamba Jiji kwenye ligi msimu huu haina matokeo mazuri ugenini kwani katika mechi 13 ilizocheza, imeshinda mbili, imepoteza nane na sare tatu.

Wakati ugenini hali ikiwa mbaya, nyumbani anagalau kidogo baada ya kushinda nne na kupoteza tatu, sare zikiwa sita katika mechi 13.