Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pluijm: Kwa Amankona Singida BS italamba dume

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Uholanzi amewahi kufanya kazi Tanzania kwa zaidi ya miaka saba vipindi tofauti, anafahamu vyema aina ya wachezaji wanaoweza kufanya vizuri Ligi Kuu Bara.

KOCHA wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm ameisifu Singida Black Stars kumsajili mshambuliaji wa Berekum Chelsea ya Ghana, Stephen Amankona, akisema iwapo itafanikiwa kukamilisha dili hilo, basi itakuwa imelamba dume.

Kocha huyo raia wa Uholanzi amewahi kufanya kazi Tanzania kwa zaidi ya miaka saba vipindi tofauti, anafahamu vyema aina ya wachezaji wanaoweza kufanya vizuri Ligi Kuu Bara.

Pluijm mabaye anaishi Ghana alisema Singida inahitaji kuimarisha kikosi kwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga na pia kucheza nafasi mbalimbali za ushambuliaji, jambo ambalo Amankona analitimiza.

“Amankona ni mshambuliaji ambaye anaweza kufanya makubwa kwenye ligi yoyote ile. Ana uwezo wa kufunga, kushambulia kutokea pembeni na pia kusaidia washambuliaji wenzake. Kama Singida wakimchukua watakuwa wamelamba dume,” alisema.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, Singida Black Stars tayari imefikia makubaliano ya awali na Amankona mwenye umri wa miaka 25, na sasa ipo kwenye mazungumzo ya mwisho na uongozi wa Berekum Chelsea ili kukamilisha usajili dirisha kubwa lijalo.

Amankona ni mchezaji aliyedhihirisha uwezo wake kwenye Ligi Kuu ya Ghana ambapo msimu huu amefunga mabao 13 katika mechi 23, huku akionyesha uwezo wa kukimbia na mpira, kutengeneza nafasi na kufunga mabao ya aina tofauti. Ana uwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa kati pamoja na winga wa kushoto au kulia.

Msimu uliopita wa 2023/2024, Amankona aliibuka kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Ghana kwa kufunga jumla ya mabao 19 katika michezo 29. Takwimu hizo zimeifanya Singida imuone kama lulu, hasa baada ya dalili za kuondoka kwa mshambuliaji wao tegemeo Jonathan Sowah.

Sowah ambaye alijiunga na Singida katika dirisha dogo la usajili akitokea Al-Nasr ya Libya, ameifungia timu hiyo mabao 11 na kuisaidia kufika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, ikiwa na pointi 53. Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa huenda akajiunga na Yanga SC au Al Hilal ya Sudan mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa duru za soka, Singida imekuwa ikifanya kazi ya kimya kimya kuhakikisha wanapata mbadala bora wa Sowah, huku wakiamini kuwa Amankona ndiye mtu sahihi wa kujaza pengo hilo.

Hata hivyo, Singida italazimika kushindana na baadhi ya klabu nyingine kutoka Afrika Magharibi ambazo pia zimeonyesha nia ya kumchukua nyota huyo, hasa kutokana na umahiri tangu msimu uliopita.