Raundi saba za presha vibonde Ligi Kuu Tanzania Bara

Muktasari:
- Timu mbili zinazoshika mkia katika Ligi Kuu Tanzania Bara zinashuka daraja na timu zinazomaliza katika nafasi ya 13 na 14 kwenye msimamo wa ligi zinacheza mechi za mchujo kupata timu moja ya kubakia kwenye ligi na nyingine ya kucheza mtoano na timu ya Ligi ya Championship
Mambo yanaonekana kutokuwa mazuri kwa timu 10 ambazo bado hazina pointi za kuzifanya ziwe katika uwezekano salama wa kubakia katika Ligi Kuu ingawa timu sita zilizopo juu kwenye msimamo wa ligi hazina presha kubwa.
Zimebaki raundi saba tu msimu kumalizika na timu hizo 10 kila moja hivi sasa hapana shaka inajipanga na kufanya tathmini ya jinsi gani inavyoweza kucha karata katika mechi zake saba zilizobakia ili iweze kunusurika na janga la kushuka daraja.
Ifuatayo ni orodha ya timu 10 zilizo katika mdomo wa mamba kwenye Ligi Kuu na tathmini ya mtego ambao kila moja inakabiliana nayo kwa raundi zilizobakia.
FOUNTAIN GATE- Pointi 28
Nafasi-07
Mechi ilizobakiza- 07
Mechi za nyumbani-03
Mechi za ugenini-04
DODOMA JIJI - Pointi 27
Nafasi-08
Mechi ilizobakiza- 08
Mechi za nyumbani-03
Mechi za ugenini-05
COASTAL UNION - Pointi 25
Nafasi-09
Mechi ilizobakiza- 07
Mechi za nyumbani-04
Mechi za ugenini-03
MASHUJAA FC - Pointi 24
Nafasi-10
Mechi ilizobakiza- 07
Mechi za nyumbani-04
Mechi za ugenini-03
KMC - Pointi 24
Nafasi-11
Mechi ilizobakiza- 07
Mechi za nyumbani-03
Mechi za ugenini-04
NAMUNGO FC - Pointi 23
Nafasi-12
Mechi ilizobakiza- 07
Mechi za nyumbani-04
Mechi za ugenini-03
PAMBA - Pointi 22
Nafasi-13
Mechi ilizobakiza- 07
Mechi za nyumbani-05
Mechi za ugenini-03
KAGERA SUGAR - Pointi 22
Nafasi-14
Mechi ilizobakiza- 07
Mechi za nyumbani-03
Mechi za ugenini-04
TANZANIA PRISONS - Pointi 18
Nafasi-15
Mechi ilizobakiza- 07
Mechi za nyumbani-04
Mechi za ugenini-03
KENGOLD - Pointi 16
Nafasi-16
Mechi ilizobakiza- 07
Mechi za nyumbani-04
Mechi za ugenini-03