Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shabiki waSimba, Arsenal ashinda Sh176.5 millioni M-BET

Shabiki waSimba, Arsenal ashinda Sh176.5 millioni M-BET

Muktasari:

  • Ushindi huo umetokana na kubashiriki kwa usahihi matokeo ya mechi 12 za soka za ligi mbalimbali kwenye droo ya perfect 12.

Shabiki wa klabu ya Simba ya Tanzania na Arsenal, Swalehe Enzi ameshinda kitita cha sh 176,470,910 kupitia mchezo wa kubashiri wa Perfect 12 wa kampuni ya M-Bet Tanzania.

Enzi ambaye ni mkazi wa Mtwara ameshinda kiasi hicho cha fedha baada ya kubashiriki kwa usahihi matokeo ya mechi 12 za soka za ligi mbalimbali duniani kwa kutumia sh1,000 tu.

Amesema kuwa amebashiri kwa kipindi cha miaka mitatu huku akishinda kiasi cha fedha kidogokidogo ingawa hakukata tamaa.

Amesema pamoja na kuwa ni shabiki wa Simba na Arsenal, bado huwa anakumbana na vikwazo katika kubashiri kwake jambo ambalo limekuwa likimwaribia ‘mkeka’ wake na ‘kuchanika’.

“Mimi ni fundi selemala na nimekuwa nikibashiri kwa kutumia madaftari au ‘counterbook’. Nimefanya hivyo kwa miaka mitatu huku nikishinda zawadi za fedha ndogo ndogo.

Sikuweza kukata tamaa kwani nimeshuhudia washindi kadhaa kupitia Perfect 12 ya M-BET wakishinda fedha mamilioni. Nilijua ipo siku na mimi nitashinda kwani hakuna ubabaishaji, natoa wito kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 18, kubashiri kupitia M-BET,” amesema Enzi.

Amesema kuwa hakuamini siku alipopigiwa simu kuwa ameshinda kiasi kikubwa cha fedha hicho ambachi atakitumia kuendeleza biashara yake na piq kuanzisha nyingine, kusomesha na kujenga nyumba.

 Meneja Masoko wa M-BET Tanzania, Allen Mushi amesema kuwa wanajisikia fahari kubwa kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia mchezo yao.

Mushi amesema kuwa Watanzania wengi wamekuwa wakibashiri na kushinda kupitia michezo yao na kufanikiwa kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.

“Huu ni mwanzo wa mwaka na tayari washindi wamepatikana. Tutaendelea kuwa nyumba za washindi na kubadili maisha ya Watanzania,” amesema Mushi.