Sichone aumaliza msimu mapema

Muktasari:
- Kinda huyo (17) ukiwa msimu wake wa kwanza kukitumikia kikosi hicho amecheza mechi 18 akifunga mabao sita na kutoa asisti nane.
MSHAMBULIAJI wa Trident FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Zambia, Mourice Sichone amesema kwa asilimia kubwa malengo aliyojiwekea msimu huu yametimia.
Kinda huyo (17) ukiwa msimu wake wa kwanza kukitumikia kikosi hicho amecheza mechi 18 akifunga mabao sita na kutoa asisti nane.
Akizungumza na Mwanaspoti, Sichone alisema ingawa Ligi hiyo haijatamatika lakini anahesabu amemaliza msimu kutokana na malengo aliyojiwekea ya kufunga angalau mabao matano.
Aliongeza kuwa kasi hiyo imempa mizuka ya kujiwekea msimu ujao kufunga angalau mabao 10 kuvuka malengo ya msimu uliopita.
“Sijajua kama nitaendelea kuichezea Trident kutokana na ofa nilizonazo, kwangu nimemaliza msimu nataka ujao nifunge walau mabao 10 tu,” alisema Sichone.
Hata hivyo, alisema matamanio yake makubwa kwa msimu ujao ni kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ‘Taifa Stars’.