Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siku 14 kuamua hatma ya Pacome Yanga

pacome Pict

Muktasari:

  • Pacome aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam baada ya kugongana na Yahya Zayd katika mchezo huo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 yakiwekwa kambani naye akifunga moja na jingine la Prince Dube, huku bao la kufutia machozi la wenyeji Azam likifungwa na Lusajo Mwaikenda.

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa siku 10 hadi 14 baada ya kuumia kifundo cha mguu (Ankle sprain).

Pacome aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Azam baada ya kugongana na Yahya Zayd katika mchezo huo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 yakiwekwa kambani naye akifunga moja na jingine la Prince Dube, huku bao la kufutia machozi la wenyeji Azam likifungwa na Lusajo Mwaikenda.

Kiungo huyo hakumaliza mchezo huo baada ya kuumia huku daktari wa timu hiyo, Moses Etutu akiliambia Mwanaspoti kuwa kiungo huyo ameumia kifundo cha mguu.

“Pacome aliumia kifundo cha mguu matarajio atakuwa nje kwa siku 10 hadi 14 maendeleo yake ni mazuri akizingatia maagizo tuliyompatia kwa kuhakikisha anapumzika kwa wakati anaweza akawahi au kuchelewa zaidi ya muda huo.”

Ni mara ya pili kwa kiungo huyo kupata shida kama hiyo na kwenye mchezo dhidi ya Azam FC kama ilivyotokea msimu uliopita ambapo aliumia pia kifundo cha mguu kwenye mchezo wa ligi timu yake ikiambulia kichapo cha mabao 2-1.


NNE KABLA YA JERAHA

Pacome kabla ya kuumia kwenye mechi tatu nyuma alizocheza Yanga imefunga mabao sita, huku kati ya mabao hayo amefunga moja kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union.

Pia alitoa pasi mbili zilizozaa mabao kwenye mchezo dhidi ya Tabora United Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 yakifungwa na Israel Mwenda, alitoa pasi kwa Clement Mzize na Prince Dube huku bao la Mwenda likitokana na mpira wa kutengwa.

Na mchezo dhidi ya Azam ambao alicheza kwa dakika 23 alifunga bao la kwanza akipokea pasi kutoka kwa Dube na bao la pili na la ushindi likiwekwa kambani na Dube.


ATAKAZOZIKOSA

Pacome atakosekana kwenye mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Stand United na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa Aprili 20 mwaka huu.

Baada ya hapo Yanga itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Namungo Mei 13 mwaka huu huenda akawa sehemu ya kikosi kutokana na idadi ya siku zilizothibitishwa na daktari Etutu kutimia.


Mechi nyingine za Yanga zilizosalia ni pamoja na Tanzania Prisons itakaychezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, dhidi ya Dodoma Jiji na kisha Yanga itakuwa timu mwenyeji na mchezo dhidi ya watani wao Simba ambayo haijajulikana utachezwa lini, baada ya Wekundu wa Msimbazi kukimbia mechi hiyo ilipopangwa kuchezwa Machi 8.