Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba v Stellenbosch.... Vita ya mabilionea CAF

SIMBA Pict

Muktasari:

  • Simba imefuzu nusu fainali kwa kuiondosha Al Masry kwa penalti 4-1, wakati Stellenbosch imeifunga Zamalek bao 1-0. Mechi ya kwanza itachezwa Aprili 20 Simba ikiwa mwenyeji kisha Aprili 27, itaenda ugenini Afrika Kusini kusaka nafasi ya kucheza fainali.

KITENDO cha Simba kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika huku ikienda kucheza dhidi ya Stellenbosch, ni wazi itakuwa vita ya mabilionea wawili wenye nguvu kubwa ndani ya timu hizo ambao ni Mohamed Dewji na Johann Peter Rupert.

Simba imefuzu nusu fainali kwa kuiondosha Al Masry kwa penalti 4-1, wakati Stellenbosch imeifunga Zamalek bao 1-0. Mechi ya kwanza itachezwa Aprili 20 Simba ikiwa mwenyeji kisha Aprili 27, itaenda ugenini Afrika Kusini kusaka nafasi ya kucheza fainali.

Mabilionea wa timu hizo, wamekuwa na nguvu kubwa iliyosababisha mabadiliko ya vikosi vya timu hizo ambavyo vimewatikisa Waarabu katika mashindano hayo msimu huu.

Hivi karibuni, Jarida la Forbes (2025) limemtaja Mo Dewji kuwa miongoni mwa watu matajiri duniani, akiwa na utajiri wa dola 2.2 bilioni sawa na Tsh 5.7 trillioni. Mo, anakuwa tajiri namba 12 Afrika na namba moja Afrika Mashariki kwa utajiri huo.

Wakati Simba ikiwa na Mo Dewji, Stellenbosch iliyoanzishwa Agosti 3, 2016, ipo chini ya umiliki wa bilionea Johann Rupert ambaye ni mfanyabiashara kama ilivyo kwa Mo Dewji, ambapo yeye makazi yake yapo nchini Afrika Kusini.

Rupert ni ni mwenyekiti wa Kampuni ya Richemont yenye makao yake makuu nchini Uswizi na kampuni ya Remgro yenye makao yake Afrika Kusini. Tangu Aprili 2010, amekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Compagnie Financiere Richemont.

Kwenye orodha ya Forbes ya 2025, Rupert na familia yake wanashika nafasi ya pili kwa tajiri Afrika, nyuma ya Aliko Dangote wa Nigeria, ikiwa na makadirio ya jumla ya thamani ya dola 15.2 bilioni na dola 17.7 bilioni kulingana na Bloomberg Billionaires Index.

Remgro Limited ni kampuni inayomiliki uwekezaji iliyoko Stellenbosch, Afrika Kusini. Ina maslahi katika benki, huduma za kifedha, bidhaa za kioo, huduma za matibabu, madini, mafuta ya petroli, vinywaji, chakula na bidhaa za utunzaji wa kibinafsi.

Bilionea huyo tangu aimiliki rasmi Stellenbosch Agosti 2018, amefanya uwekezaji mkubwa na kukifanya kikosi cha timu hiyo kuwa na thamani ya Sh33 bilioni za Kitanzania kulinganisha na cha Simba chenye thamani ya Sh6.4 bilioni.

Takwimu hizo ni kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarket.