Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaipa Yanga Sh1.8 bilioni

Bilioni Pict

Muktasari:

  • Yanga ushindi huo wa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara uliochezwa Juni 25, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam umewafanya wachezaji wa kikosi hicho kuvuna bonasi Sh1.8 bilioni.

YANGA ina raha sana. Inatamba na ubingwa wa Ligi Kuu Bara iliyouchukua mbele ya mtani wao, Simba na mchezo huo ukawapa kitita kikubwa cha fedha mastaa wa mabingwa hao.


Yanga ushindi huo wa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara uliochezwa Juni 25, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam umewafanya wachezaji wa kikosi hicho kuvuna bonasi Sh1.8 bilioni.


Ipo hivi. Ushindi wa mechi hiyo ya juzi ya kiporo kilichokuwa kimeahirishwa mara mbili, Machi 8 na Juni 15, wachezaji wa kikosi hicho, kwanza walivuna kiasi cha Sh500 milioni kutoka kwa mabosi  wa klabu hiyo, fedha hizo zikitokana na ahadi ya viongozi chini ya Rais Injinia Hersi Said.

Kama haitoshi, Bilionea Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ naye akaweka mezani kiasi kama hicho cha Sh500 milioni ikiwa ni ahadi kwa ushindi wa Dabi hiyo ya marudiano.

Fedha zote hizo zimewafanya wachezaji na benchi lao la ufundi kujikusanyia jumla ya Sh1 Bilioni kwa ushindi huo dhidi ya Simba na ubingwa wa msimu huu.

Hii inakuwa bonasi kubwa zaidi kwa Yanga msimu huu kwa mchezo wa Dabi na ahadi hiyo ilitoka mapema kwenye mazoezi ya mwisho ya timu hiyo yaliyofanyika Juni 24, 2025 Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ikumbukwe Yanga msimu huu imeifunga Simba mara tatu ikianzia katika mechi ya kwanza ya Ngao ya Jamii iliposhinda kwa bao 1-0, wachezaji wa timu hiyo wakapata bonasi ya Sh300 milioni.

Kama haitoshi, timu hizo zilipokutana tena katika mechi ya kwanza ya Ligi ambayo Yanga ikashinda kwa bao 1-0, wachezaji wakavuna bonasi ya Sh500 milioni na kufanya jumla kwa mechi hizo tatu kujikusanyia Sh1.8 bilioni.

Staa mmoja wa Yanga amefichua, walilazimika kukomaa kwenye mechi hiyo ili kujipatia fedha hizo kutoka kwa viongozi wa klabu.

“Unaona tulivyokuwa tunahamasishana kuanzia tunatoka kambini kwamba jamani hizi ndio fedha za kufungia msimu tukafanye mambo makubwa na familia zetu, kama tusingeshinda tungeumia sana,” alisema staa huyo anayecheza eneo la kiungo.

Wakati wachezaji wa Yanga wanachekelea, wenzao wa Simba watakuwa kwenye maumivu makali kwani wamekosa kuvuna bonasi ya Sh600 milioni.

Mabosi wa Simba walipokutana na timu hiyo kabla ya mchezo wakatoa ahadi ya kuwapa wachezaji kiasi cha Sh600 milioni ambazo waliambiwa zipo tayari zinawasubiri endapo wakiifunga Yanga na kuwa mabingwa wa Ligi kwa mara ya kwanza kutokana na kuukosa misimu mitatu mfululizo tangu ilipoubeba mara ya mwisho msimu wa 2020-2021.