Simba yang'ara tuzo za Machi

Muktasari:
- Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa imekusanya pointi 57 katika mechi 22.
Dar es Salaam. Tuzo za Ligi Kuu mwezi Machi zimetawaliwa na Simba ambayo imenyakua tuzo ya Kocha Bora wa mwezi na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi.
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) leo imeeleza kuwa kocha bora wa Machi ni Fadlu Davids na mchezaji bora ni Steven Mukwala.
“MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, Steven Mukwala amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2024/25, huku Fadlu Davids pia wa Simba akichagullwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.
“Mukwala alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiwashinda Elie Mpanzu wa Simba na Paschal Msindo wa Azam alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi utiofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
“Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo miwili ambayo Simba ilicheza mwezi huo na kufunga mabao manne, huku matatu akifunga katika mchezo mmoja (hat-trick). Mukwala alicheza dakika 152 za michezo miwili.
Kwa upande wa kocha Davids aliyeingia fainali na Rachid Taoussi wa Azam na
David Ouma wa Singida Black Stars, aliiongoza Simba kushinda michezo yote miwili iliyocheza mwezi huo. Simba ilifunga Dodoma Jiji mabão 6-0 na Coastal Union mabao 0-3, hivyo kuendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi,” imefafanua taarifa hiyo.
Bodi ya Ligi pia imetaja washindi wa tuzo nyingine kwa mwezi Machi.
“Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Sokoine Mbeya, Modestus Mwaluka kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Machi kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.
“Wakati huo huo Kamati ya Tuzo za TFF, imemchagua Mwani Thobias wa Mbeya
City kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Machi wa Ligi ya NBC Championship 2024/25,
huku Awadh Juma wa MLibwa Sugar akichaguliva Kocha Bora wa mwezi huo.
“Thobias aliyeingia fainali na Magata Charles wa Mtibwa Sugar na Selemani Richard wa Stand United, alionesha kiwango chenye mendelezo, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matano kwa dakika 325 alizocheza za michezo minne.
“Kwa upande wa Awadh aliyeingia fainali na Mohamed Ismail wa TMA na Juma
Hussein wa Stand United, aliiongoza Mtibwa Sugar kushinda michezo mitatu kati ya minne iliyocheza na kuendelea kubaki kileleni kwenye msimamo wa ligi,” imefafanua taarifa hiyo ya TPLB.