Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu ya taifa ya Futsal kuanza na Madagascar

TWIGA Pict

Muktasari:

  • Mashindano hayo pia yatatumika kama hatua ya kufuzu Kombe la Dunia la Wanawake la Futsal la Fifa 2025 litakalofanyika nchini Ufilipino kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 7, mwaka huu.

ALHAMISI wiki hii Timu ya Taifa ya Wanawake ya Futsal  itashuka Uwanja wa Salle Moulay Abdellah jijini Rabat, Morocco kwenye mchezo wa kwanza wa makundi dhidi ya Madagascar kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika la Futsal kwa Wanawake mwaka huu.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) yatafanyika Morocco kuanzia Aprili 22 hadi 30.

Mashindano hayo pia yatatumika kama hatua ya kufuzu Kombe la Dunia la Wanawake la Futsal la Fifa 2025 litakalofanyika nchini Ufilipino kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 7, mwaka huu.

Timu tisa kutoka Afrika zitachuana kumpata bingwa atakayewakilisha Kombe la Dunia.

Tanzania imepangwa kundi C na Madagascar, Senegal huku kundi B likiwa na Angola, Misri na Guinea ilhali A likiongozwa na waandaaji wa mashindano hayo Morocco, Cameroon na Namibia.

Baada ya mchezo wa kwanza na Madagascar, Aprili 26 Tanzania itamalizana na Senegal mchezo wa mwisho wa makundi.

Akizungumza baada ya kuwasili Casablanca, Morocco, mkuu wa msafara Zena Chande alisema: "Tumefika salama Casablanca tuko vizuri hakuna majeruhi kila mchezaji yuko vizuri na wameahidi watafanya vizuri na kujifunza kwa wenzao wenzetu wameanza muda mrefu.

"Tulikuwa kambini kwa takribani mwezi mmoja, matumaini ni makubwa kutokana na ubora wetu kwenye ukanda wa Afrika Masahariki."

Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo kufanyika Afrika lakini kwa duniani hii ni mara ya pili baada ya kufanyika 2010 nchini Hispania ambapo Brazil ilitwaa ubingwa huo.

Katika Bara la Ulaya, UEFA ilizindua mashindano ya kwanza ya Futsal kwa Wanawake (UEFA Women's Futsal EURO) mnamo Februari 2019, yakihusisha timu kutoka mataifa manne, Uhispania, Ureno, Urusi na Ukraine.