Ulimboka: Kiiza ni bora zaidi ya Jaja

Hamis Kiiza.PICHA|MAKTABA
Muktasari:
- Mwakingwe alisema: “Maximo hatoweza kufaidi chochote kwa Jaja iwapo anamuweka Kiiza kama chaguo la pili la straika mmaliziaji.
STRAIKA wa zamani wa Simba Ulimboka Mwakingwe, amesema kuwa Kocha Marcio Maximo anachemka kumpa kipaumbele Genilson Santos ‘Jaja’ badala ya Hamis Kiiza kikosini Yanga.
Mwakingwe alisema: “Maximo hatoweza kufaidi chochote kwa Jaja iwapo anamuweka Kiiza kama chaguo la pili la straika mmaliziaji.
“Hauwezi kumfananisha Kiiza na Jaja, Jaja bado hawezi kufanya majukumu kama Kiiza.Kiiza ana kila uwezo hasa wa kufunga magoli, pia anaweza kucheza pasi za mwisho lakini pia ni mjanja anapokuwa na mpira katikati au akitokea pembeni ya uwanja huku akikimbia kwa kasi.
“Jaja hana kipya tena kwa taarifa na jinsi nilivyomuona akicheza ni mchezaji wa kusubiria si mpambanaji. Maximo anampa nafasi ya kwanza kwenye kikosi chake akiamini kuwa ndiye mchezaji anayeendana na mfumo wake, lakini hawezi.”