Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vimwana 30, kuwania zawadi ya Sh18milioni Dar!

Mwaka huu Tanzania itawakilishwa na mrembo kutoka Dodoma, Happiness Watimanya aliyeshinda taji la mwaka jana kwenye ukumbi huo huo.

Muktasari:

Warembo hao watawania zawadi ya kwanza na tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia mwakani.

MASHINDANO ya kumtafuta mrembo wa Tanzania ‘Redds Miss Tanzania 2014’ yatafanyika leo Jumamosi kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha warembo 30.

Warembo hao watawania zawadi ya kwanza na tiketi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia mwakani.

Mwaka huu Tanzania itawakilishwa na mrembo kutoka Dodoma, Happiness Watimanya aliyeshinda taji la mwaka jana kwenye ukumbi huo huo.

Pia watashindania zawadi ya kwanza ya Sh18 milioni zilizotolewa na wadhamini wakuu wa shindano hilo, zawadi hiyo ni tofauti na mwaka jana ambapo mrembo alipewa fedha taslimu na gari aina ya IST yenye thamani ya Sh Milioni 16.

Mkurugenzi wa kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga, alisema jana Ijumaa kuwa wanaamini kuwa kuna watu wengine gari si kitu cha lazima kwao na ndiyo maana wamempa uhuru wa kuchagua nini cha kufanya.

Mbali ya zawadi hiyo ya mshindi wa kwanza, mshindi wa pili atazwadiwa kitita cha Sh6 milioni wakati wa tatu atapewa Sh4.2 milioni na wa nne ataondoka na Sh3.2 milioni. Mshindi wa tano atapewa Sh2.2 milioni na watakaomaliza ndani ya 15 bora wataondoka na Sh1.2 milioni kila mmoja. Warembo wengine 15 watazawadiwa Sh700,000 kila mmoja ikiwa ni zawadi ya kifuta jasho.

Warembo watakaopanda jukwaani ni Lilian Kamazima (Arusha), Martha John (Iringa), Nasreen Abdul (Ilala), Salama Saleh (Temeke), Patricia Pontian(Temeke), Sophia Masei (Elimu ya Juu), Elizabeth Tarimo (Lindi), Dorice Mollel (Singida), Naomi Kisaka (Ilala), Sitti Mtemvu (Temeke), Rachel Clavery (Geita), Maria Shilla (Kinondoni), Evelyn Baasa (Arusha), Mariam Hussein (Open University) na Lucy James kutoka Morogoro.

Wengine ni Sabina Thomas (Ilala), Happiness Samuel (Kilimanjaro), Nidah Katunzi (Mtwara), Maurine Godfrey (Njombe), Nicole Sarakikya (Shinyanga), Mary Emmanuel (Shinyanga), Doreen Beno (Kinondoni), Doreen Robert (Mwanza), Camilla John (Kinondoni), Lilian Timothy (Higher Learning), Happiness Sosthenes (Ilala), Queen Latifa hashim (Knondoni), Junes Ndalima (Higher Learning), Jihan Dimachk (Ilala) na Naba Magambo wa Ruvuma.

Mashindano hayo yatapambwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee wakati Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Juma Nkamia atakuwa mgeni rasmi.