Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Viongozi Yanga watajiwa kocha mpya

BAADA klabu ya Yanga kuachana na kocha wake Cedric Kaze, wadau wa soka wamewashauri viongozi wa Yanga kutafuta kocha mzawa kwa kipindi hiki kilichosalia.

Uongozi wa Yanga jana uliamua kuvunja benchi zima la ufundi la timu hiyo baada ya kutoka sare 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Wadau wa soka nchini wamewashauri uongozi wa klabu hiyo kutojichanganya kuleta kocha kutoka nje kwa kipindi hiki kama wanataka Ligi.

Aliyewahi kuwa beki wa timu hiyo, Bakari Malima 'Jembe Ulaya' alisema kwa upande wake anaona aende mzawa kama Mecky Maxime asaidiane na Juma Mwambusi anaamini watawavusha katika kipindi hiki.

"Mwambusi amekaa na hawa wachezaji lakini pia anawafahamu vizuri, Mecky analijua soka la Bongo kwahiyo nazani ni wakati sahihi wao kupewa kwa muda timu waende nayo mpaka mwisho wa msimu, baada ya hapo ndio watajua waendelee nao au vipi".

Kwa upande wa Herry Morris ambaye aliwahi kuwa mshambuliaji katika timu hiyo, alisema kocha mzawa ndio wakati wake kipindi hiki na wasithubutu kuleta mgeni watazidi kujivuruga.

"Yanga kipindi hiki wanahitaji kocha mzawa ndio anaweza kuwavusha kutoka hapa kwenda sehemu nyingine, akija mgeni yatakuwa ni mambo mengi".